VAR Stop, Sub Tano - IFAB

Timu zitaruhusiwa kufanya mabadiliko matano ya wachezaji kwa mechi baada ya  International Football Association Board (IFAB) kufanya mabadiliko ya muda kwenye sheria za mpira ili kuendana hali ya kurejea kwa Ligi baada ya Corona kulazimisha Ligi nyingi kusimama.

FIFA ilishauri sheria hiyo kufanyiwa mabadiliko na IFAB, ambao ndio wenye jukumu la sheria za mchezo, wakati wachezaji watakapocheza mechi kwa muda maalum kipindi cha miezi ya kiangazi.

Timu zitakuwa na nafasi tatu wakati wa mechi kufanya mabadiliko na pia wakati wa mapumziko, ili kuzuia mpira kusimama bila kila mara. Katika mashindano yenye muda wa ziada pia itakuwa hivyo, mchezaji ambae hajaingia ataruhusiwa kuingia.

Mabdiliko haya ya sheria yameanza mara moja, lakini kwenye mashindano binafsi wataamua kama wataiga mfumo huu. Itatumika Bundesliga, ambayo imepangwa kuanza May 16 japo bila mashabiki.

Kwasasa, La Liga na Shirikisho la Hispania wamekubaliana kutumia sub tano kwenye mechi zote zilizosalia, ambayo inatarajia kuanza Juni.

IFAB imesema mabadiliko haya yatatumika kwenye mashindano ambayo yamepangwa kumalizika kabla mwaka huu haujaisha, na mapitia yatafanyika hapo baadae kuona kama tunaweza kuendelea na mabadiliko hayo msimu ujao.

IFAB wamebadili sheria zake kuhusu VAR kuruhusu mashindano yote ambayo yanatumia teckonolojia hiyo kuacha kutumia, watakapoendelea na msimu.

Premier League itajadili kuhusu mabadiliko hayo na vilabu, japo kuna lengo la kuachana na VAR.

39 Komentara

    IFAB Sheri’s zao zko vzur kulingana kipindi hiki

    Jibu

    Ifab Sheria zao zinaua ladha ya mpira

    Jibu

    Aisee bora VAR ifutwe tu inaharibu sana radha ya mpira

    Jibu

    Itabid tu kufanya mabadiliko kutokana na kipind hk kigum no way

    Jibu

    AVR imekuja me kumaliza Radha yote ya mpira sheria mpya kila kukicha

    Jibu

    Itakuwa safi sana.

    Jibu

    Iwe ivyo tu ilaumiwe corona

    Jibu

    itatoa nafasi ya wachezaji wengi

    Jibu

    itakuwa poaw

    Jibu

    Bora VR zinazingua sana

    Jibu

    Kwangu me VAR ufutwe kabisa ..kwasababu ikiwepo inanyima radha ya mchezo .

    Jibu

    VAR isifutwe inasaidia Sana

    Jibu

    Bora VAR ifutwe tu

    Jibu

    VAR isifutwe inasaidia sana

    Jibu

    VAR ililetwa kumusaidia refa lakini wakati fulani maamuzi yanakuwa na utata mkubwa mno. Hakuna sababu ya kuendelea nayo. Asante IFAB

    Jibu

    Sasa si waifute tu jamani

    Jibu

    Itakuwa vizuri saana

    Jibu

    Bora var ifutwe

    Jibu

    sab tano? aisee itakaa poa sana alafu na hiyo VAR itolewe tuu inazingua japo wakati mwingine inasaidia

    Jibu

    Bora tu mabadiriko yafanyike hakuna namna

    Jibu

    Itakuwa poa sana

    Jibu

    Itakuwa vizur sana

    Jibu

    Safi sn

    Jibu

    IFAB wamefany jamb la maana sana kwa kpnd hch dunia inabambana na janga la korona

    Jibu

    IFAB wamefanya Jambo la busara kubadili Sheria kwa kipindi hiki Cha janga hili la COVID-19

    Jibu

    wapunguze sub bana

    Jibu

    Wamefanya maamuzi mazuri ili viwango vya wachezaji wetu visishuke.

    Jibu

    Mi kote kote naona sawa muda mwingine nzur muda mwingine inazngua

    Jibu

    sheria znaua soka bhn

    Jibu

    Kisimamishwa kwa VAR sio jambo zuri sana japo kunawakati inaleta kizungumkuti katika maamuzi lakini ni tekinolojia bora sana kwa upande wa kuwasaidia marefa katika kufanya maamuzi.

    Jibu

    VAR ipo poa sanaa

    Jibu

    Bora var ifutwe

    Jibu

    Itakuwa vzr sana

    Jibu

    Itakuwa vzr sana

    Jibu

    VAR .isifutwe

    Jibu

    Waache 2

    Jibu

    Kila kitu kina uzuri wake na kasoro zake, km kuna muda tunaona VAR inafanya sahihi na tunafurahia iwenye tushindwe kukubali mapungufu yake?

    Jibu

    Var ilikuwa inapunguza burudani sana

    Jibu

    Itakuwa vzr Sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.