VAR  inayosimama kwa kirefu cha (Video Assistant Referee) imeleta utata hapo jana kwenye mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza kati ya Westham dhidi ya Bournemouth ambapo Vijana wa Westham walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Bournemouth.

 

 VAR Yaleta Utata Kwenye Ushindi wa Westham Dhidi ya Bournemouth.

Bao la kwanza kwa Westham lilifungwa na Kurt Zouma katika dakika ya 45 + 1 likiwa ni bao lake kwanza msimu huu tangu alipofunga Novemba 2021 liliruhusiwa na VAR kuwa bao licha ya mpira kugusa mikono ya wachezaji kama vile Thilo Kehrer.

Wakati wamerejea kipindi cha pili, mpira ukiendea kumalizika Said Benrahma alifunga bao la penati ambalo nalo pia lilikuwa na ukakasi huku VAR ikiamua kuwa mchezaji wa Bournemouth  Zemura alishika mpira huo kwa mkono wakati krosi ikipigwa na kufanya matokeo kuwa 2-0.

Stockley Park alitoa neno na kusema kuwa  kwa sababu mpira wa mikono haukuwa wa makusudi, na haukuwa na uelekeo  moja kwa moja kwenye goli, kwamba iliruhusiwa kusimama, huku wachezaji kushangazwa na matukio hayo yanayoendelea.

 VAR Yaleta Utata Kwenye Ushindi wa Westham Dhidi ya Bournemouth.

Vilevile kocha mkuu wa Bournemouth, Gary O’Neil alikasirishwa na uamuzi huo huku akiona kuwa VAR ilikosea kufanya maamuzi hayo hivyo mabao hayo hayakusatahili kusimama.

Benrahma sasa amaefikisha mabao matatu msimu huu na West Ham wamepanda hadi nafasi ya 10 na kuingia katika nusu ya juu kwa mara ya kwanza msimu huu

Ilikuwa mwisho mkali kwa vipindi vyote viwili vya mechi ambayo West Ham ilifanya kazi ngumu kutafuta njia ya kupita kwenye safu ya miili kwenye safu ya ulinzi ya Bournemouth.

 VAR Yaleta Utata Kwenye Ushindi wa Westham Dhidi ya Bournemouth.

Kocha wa Westham Moyes amelalamika hivi karibuni kwamba simu nyingi zilikuwa zikienda kinyume na upande wake kuhusu mfumu huo wa kuangalia kwenye VAR  lakini hapo jana alikuwa na bahati.

West Ham mpaka sasa wameshinda mechi 5 mfululizo wakiwa nyumbani katika mshindano yote huku wakianza kujitafuta baada ya kuwa na matokeo ambayo hayaridhishi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa