Varane Apiga Chini dili la Saudia

Beki wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ufaransa Raphael Varane inaelezwa amepiga chini ofa za vilabu mbalimbali kutoka nchini Saudia Arabia.

Beki Raphael Varane amekua akifuatiliwa na vilabu kadhaa kutoka nchini Saudia Arabia, Lakini beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa inaelezwa hana mpango wa kujiunga na timu yeyote kutoka nchini Saudia wakati huu akili yake ipo Man United.varaneLicha ya beki huyo kuonesha kutohitaji kwenda nchini Saudia Arabia kucheza ligi ya Saudian Pro League, Lakini pia Manchester United inamuona kama mchezaji wake muhimu na hawana mpango wa kumuachia mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo.

Beki Varane ambaye amejiunga na klabu hiyo mwaka 2021 akitokea Real Madrid ya nchini Hispania amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu hiyo kwa kipindi chote ambacho amekua ndani ya klabu ya Manchester United.varaneBeki huyo wa zamani wa Real Madrid na Stade de Rennes ya Ufaransa anaamini bado ana uwezo wa kupambana barani ulaya katika levo ya juu na ndio sababu kubwa imemfanya kugomea ofa mbalimbali kutoka nchini Saudia Arabia ambazo zinakimbiliwa na wachezaji wengi kwasasa.

Acha ujumbe