Varane Kukosekana Wiki Sita

Beki wa klabu ya Manchester United Raphael Varane ana uwezekano mkubwa wa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita baada ya kupata majeruhi wikiendi iliyopita dhidi ya Nottingham Forest.

Klabu ya Manchester United mpaka sasa imeweka wazi kua Varane atakosekana katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wikiendi hii dhidi ya klabu ya Arsenal, Lakini vyanzo mbalimbali vinaeleza beki huyo huenda akakosekana kwa wiki sita.varaneManchester United kwasasa hali sio nzuri sana kwenye timu hiyo kutokana na kupata majeraha wengi haswa katika safu ya ulinzi kwani siku kadhaa walipata taarifa ya kuumia kwa beki wake wa kushoto Luke Shaw.

Beki huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa atawafanya zaidi Man United wafikirie kuingia sokoni kutafuta beki wa kati ambaye walikua wanamfukuzia sokoni, Lakini kubaki kwa beki Maguire kukaondoka mpango huo japo mpango unaweza kurejea baada ya Varane kuingia.varaneBeki huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara tangu ajiunge na timu hiyo na inaweza kua sababu ya klabu hiyo kuingia sokoni kutafuta beki mpya kabla ya dirisha la usajili kufungwa ambapo imebaki siku tatu.

Acha ujumbe