Raphael Varane; Ofa ya United Yabuma

Manchester United wameripotiwa kuwasiliana na Real Madrid na kuwasilisha ofa yao ya kwanza kwa beki Raphael Varane.

Staa huyo wa zamani wa Lens kwa sasa yupo na timu ya Ufaransa kwa kampeni yao ya Euro 2020, lakini uvumi wa hatma yake unaendelea kushika kasi wakati kukiwa na sintofahamu juu ya ya mkataba wake huko Bernabeu.

Varane kwa sasa anatarajiwa kuwa wakala huru baada ya miezi 12 na haonekani kufikiria kuongezea muda, ikiashiria kuwa Los Blancos wanatarajiwa kuingiza pesa wakati wa dirisha hili la uhamisho wa majira ya joto.

Mitano Tena kwa Raphael Varane Madrid au United?

Man United wametajwa kumfuatilia Mfaransa huyo kama mshirika wa muda mrefu wa Harry Maguire, na Manchester Evening News sasa inadai kwamba Mashetani Wekundu wamejitokeza na zabuni ya awali ya pauni milioni 50.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa zabuni hiyo ilirudishwa, wakati Real Madrid wakitaka kitita cha pauni milioni 80, lakini kutokana na hali ya mkataba wake, United wanatarajia Los Blancos watapunguza bei yao wakati wa mazungumzo.

Chelsea na Paris Saint-Germain pia wanasemekana wako kwenye mbio za kusaka saini ya Varane, ambaye ameshinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa na mataji matatu ya La Liga kwa miaka 10 akiwa huko Madrid.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

Acha ujumbe