Verratti Kuwakosa Uingereza na Hungary

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italy Roberto Mancini amethibitisha kuwa kikosi chake kitamkosa kiungo wa Paris Saint German  Marco Verratti katika mechi zao za ligi ya Mataifa dhidi ya England na Hungry.

 

Verratti Kuwakosa Uingereza na Hungary

 

Marco Verratti aliumia katika kipindi cha pili cha mchezo wao dhidi ya Lyon siku ya Jumapili baada ya kuumia nyama za miguu kwenye mchezo ambao Psg walishinda kwa bao 1-0. Mkufunzi wa Psg alisema baada ya mchezo huo kuwa Verratti mwenye miaka 29 atachelewa kujiunga na kikosi cha Italia yake akachunguzew jijini Paris siku ya Jumatatu.

Mancini kwasasa anajiandaa na ziara ya Ijumaa ya Uingereza na safari ya Hungary siku tatu baadae bila Verratti, huku David Frattes wa Sassuolo akiwa katika mstari wa kuitwa, huku kukiwa na habari njema zaidi kuhusu Sandro Tonali wa Milan na Matteo Politano wa Napoli.

“Verratti hapatikani, amepata jeraha” Mancini alisema katika mkutano wa Waandishi wa habari siku ya Jumatatu .”Labda nitampigia Frattes kuchukua nafasi yake.

 

Verratti Kuwakosa Uingereza na Hungary

Italy ilitoka sare na Ujerumani na Uingereza katika mechi zao na kuifunga Hungary katika mechi tatu za kwanza za kundi A3, kabla ya kufungwa 5-2 katika mechi ya mchujo na Ujerumani mara ya mwisho.

Mabingwa hao watetezi wa ligi ya Mabingwa Ulaya wanashika nafasi ya tatu, pointi mbili nyuma ya vinara Ujerumani na pointi tatu mbele ya Uingereza katika msururu wa kushuka daraja.

Manchini alisema kuwa “Lolote linaweza kutokea katika kundi hili.” “Haikuwa ni furaha kupoteza kwa 5-2 mchezo uliopita lakini hata hivyo niliona dalili chanya. aliendelea kwa kusema wakati mwingine unahitaji mechi kama hizi ili uweze kuimarika, na hiyo ilikuja mwishoni mwa msimu uliopita tulipocheza mechi nyingi. Lakini wachezaji wachanga wamepata uzoefu na tumefanya vyema kwa ujumla kwa pointi tano zilizokusanywa.

 

Verratti Kuwakosa Uingereza na Hungary

Acha ujumbe