Klabu ya Simba imetangaza viingilio vya mechi yao ya marudiano nyumbani dhidi ya Kaizer Cheifs, Jumamosi ijayo ambapo kiingilio cha chini kitakuwa ni Sh 5,000.
“Uongozi wa Simba umeomba kwa CAF watuongeze idadi ya mashabiki kutoka 10,000 wa mwanzo hadi 20,000 au 30,000 hivyo ndio tunasubiria majibu na tunaamini watatukubalia kwa hilo ukizingatia kwa sasa hali ya Corona imepoa kidogo baadhi ya nchi mashabiki wameanza kuingia viwanjani”.
Viingilio katika mchezo huo vitakuwa ni Sh 40,000 kwa VIP A, Sh 25,000 kwa VIP B na C na mzunguko itakuwa ni Sh 5,000.
Katika hatua nyingine, Mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mchezo huo baina ya Simba na Kaizer Chiefs.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Shakila
Safi San Simba
Magdalena
Wasije wakatuangusha tu
Sauda
Ebwana ndiyo