Wakati baadhi ya klabu zikilia na suala zima la ukata na kuangalia namna ya kujikwamua na sakata hilo kila leo, leo tunajuletea vikosi ambavyo vina thamani kubwa na ya aina yake katika bara la Ulaya. Hilo linatokana na mapato yao, aina ya wachezaji na aina za ligi ambazo vikosi hivyo vinashiriki.

Manchester City, Pep ameweza kuwa nguzo ya mafanikio makubwa katika klabu hiyo kwa kutengeneza kikosi ambacho ni kikubwa kwa taifa hilo la Uingereza. Mbali na hilo ana majina makubwa sana ndani ya kikosi chake. Kuwa na watu kama De Bruyne na Sterling ni jambo ambalo ni kubwa sana kwake, utajiri wa kikosi hicho ni takribani £1.14 bilioni.

Real Madrid, hawa wameweza kupanda nafasi ya juu baada ya kuwapiku Barcelona kwa wakati huu. Hilo linatokana na usajili ambao wameufanya klabubi hapo. Kutua kwa Hazard kumewafanya kukaa imara juu ya Barcelona. Ubora na uthamani wao unafikia £1.07 bilioni ikiwa ni £40 milioni mbele ya mahasimu wao.

Barcelona, kikosi hicho ambacho hata wakimkosa Neymar au wakiwa nao hawashuki katika nafasi za juu kuna majina yenye thamani ndani yake kama Lionel Messi, Griezmann ambaye ni ingizo jipya na Dembele ambao wanakipa heshima kubwa kikosi hicho. Hadi sasa wana thamani kubwa sana ambayo inakadiriwa kuwa ni £1.03 bilioni.

Liverpool, mbali na kuwa na watu kama Mo Salah, Sadio Mane na Van Dijk ambao wanathamani kubwa ndani ya kikosi hicho cha mabingwa hao wa klabu bingwa Ulaya. Lakini wachezaji wake wengi wanachukua kiwangi cha chini ambacho hakivuki £45M. Lakini pamoja na hilo wana thamani ya jumla ya £959.18M.

PSG, kuwepo kwa majina makubwa kama Mbappe, Neymar ambao walikuwa wanakipa hadhi kikosi hicho kwa siku za nyuma; lakini pia kuwasili kwa Icardi kumeongeza thamani kubwa sana kikosini hapo kwa siku za hivi karibuni. Matajiri hao wa Ufaransa wana thamani kubwa sana inayokadiriwa kufikia £949.5M.

Klabu nyingine zinazotengezeza idadi ya klabu kumi ambazo vikosi vyao vina thamani ya juu ni Tottenham (£881.55M) ambao nafasi yao ya kutinga fainali ya klabu bingwa iliwapa heshima kubwa. Ambapo kuwasili kwa Ndombele, Lo Celso, Sessegnon na wengine ambao walikuwepo kama Kane na Eriksen na Dele. Bayern Munich (£779.99M), Juventus (£777.60M), Atletico Madrid (£737.69M), Chelsea (£697.50M). Lakini Manchester United wapo nafasi ya 11 wakiwa na £644.63M.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa