Viktor Gyokeres: Nitamaliza Msimu Hapa Sporting CP

Mshambuliaji matata raia wa kimataifa wa Sweden Viktor Gyokeres ambaye anafanya vizuri sana kwasasa amesema hana mpango wa kutimka ndani ya klabu ya Sporting Cp kutoka nchini Ureno katika dirisha dogo mwezi Januari.

Viktor Gyokeres amekua akihusishwa kutimka klabuni hapo katika dirisha dogo la mwezi Januari huku vilabu mbalimbali vikiwa vinamfukuzia saini ya mshambuliaji huyo kwa karibu sana, Lakini mshambuliaji huyo amesisitiza hana mpango wa kuondoka kwenye klabu hiyo katika dirisha dogo la mwezi Januari.viktor gyokeres“Nataka kumaliza msimu huu nikiwa Sporting. Napapenda hapa.”

“Klabu mpya? Tutaona wakati ukifika. Ninataka kucheza, hilo ni jambo muhimu… na pia kutakuwa na mambo mengine ya kuzingatia.”

Kutokana na kiwango bora ambacho amekua nacho mshambuliaji Viktor Gyokeres kwasasa licha ya kuweka wazi hatatimka ndani ya klabu hiyo mwezi Januari, Lakini ni wazi hatasalia klabuni hapo kwenye dirisha kubwa na tetesi zinasema anaweza kuungana na kocha wake ambaye amemfanya kua bora Ruben Amorim ambaye amejiunga na klabu ya Manchester United lakini pia vilabu vingine vimekua vikiwinda saini yake kwa karibu.

Acha ujumbe