Vinicius Jr amewaibua wachezaji mbalimbali wa kibrazil hii ni baada ya aina yake ya ushangiliaji kukemewa na vyombo vya habari mbalimbali nchini Hispania.

Mchezaji huyo raia wa Brazil ambae amekua na kiwango bora sana toka msimu uliomalizika ameibua mjadala mkubwa baada ya kufunga bao katika mchezo wa mwisho wa juma lililopita dhidi ya Real Mallorca na kushangilia kwa aina ya kucheza dansi kitu kilichofanya vyombo vya habari nchini Hispania kukemea kitendo hicho na kusema aina hiyo sio nzuri ya kushangilia kama nyani ni kama imekosa nidhamu na inawakera wengine.

vinicius jrKutokana na vyombo vya habari nchini humo kumtaka mchezaji huyo aache aina hiyo ya ushangiliaji imewaibua nyota mbalimbali wa taifa hilo ambao wameonesha kumpa ushirikiano staa huyo asiache kushangilia hivo na mastaa hao ni kama Thiago silva wa Chelsea,Raphinha wa Barcelona,Lucas pacqueta wa West Ham Neymar wa PSG pamoja na gwiji kabisa ambae ametumia mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuonesha hajapendezwa na ambacho vyombo vya habari nchini Hispania Vinafanya hivo kumtaka Vini kuendelea kudumisha utamaduni.

Staa huyo nae amekua akijibu machapisho hayo ya mastaa wenzake wa Kibrazil kuonesha ataendelea kudumisha aina yake ya ushangiliaji kitu ambacho ni kama utamaduni kwa jamii ya kibrazil kufunga bao na kushangilia kwa namna ya kucheza dansi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa