Viongozi wa Vilabu Wakubali Kuwakata Wachezaji 30%

Ligi Kuu ya Uingereza itakutana na Chama cha wachezaji wakulipwa (PFA) Jumamosi ili kujadili kuhusu kuwakata wachezaji 30% kipindi cha mlipuko wa Corona.

Viongozi wa vilabu 20 wamekutana Ijumaa, ili kujadili kupunguza mishahara kwa 30% kwa mwaka.

Vilabu kama Tottenham na Newcastle,tayari wamekata mishahara wafanyakazi ambao sio wachezaji wakati wachezaji wakipata mshahara kamili.

Katika kikao kicho hicho, imekubaliwa kuwa mechi hazitaanza mwanzoni mwa Mei na msimu utaendelea watakapoona ni salama kufanya hivyo.

Taarifa ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyotolewa Ijumaa inasomeka: “Baada ya kusimama kwa muda msimu wa 2019/2020 kabla ya mechi kurejea inabidi tulinde ajira katika michezo, viongozi wa vilabu wamekubaliana kupunguza mishahara ya wachezaji kwa 30% kwa mwaka.

Viongozi wa Ligi Kuu ya Uingereza walikuwa na lengo la kumalizia msimu wa 2019/2020 lakini bado haijathibitishwa kama mechi zitarejea baada ya tarehe 30 Aprili, tarehe ambayo awali ilitajwa na FA kuwa mechi zimehairishwa hadi tarehe hiyo.

Wakati huo huo UEFA wametoa tahadhari kwa wanachama wake kuwa hawatakiwi kumaliza msimu katika kipindi hichi na kusema hawatatambua mabingwa hao.

Jurgen Klopp's Liverpool need just two wins to secure the Premier League title
Liverpool wanahitaji ushindi kwenye mechi mbili kujihakikishia ubingwa

Liverpool wapo alama 25 kileleni mwa msimamo wa ligi wakihitaji ushindi wa mechi mbili tu ili kujihakikishia ubingwa kabla ya ligi kusimamishwa Machi 13.

 

2 Komentara

    Safi

    Jibu

    Gud

    Jibu

Acha ujumbe