Virgil Van Dijk Aanza Mazoezi Mepesi

Taarifa njema kwa mashabiki wa Liverpool ni kwamba beki kitasa wa timu hiyo Virgil Van Dijk anatajwa kuanza kufanya mazoezi mepesi yatakayomsaidia kurejea kwenye ubora wake wa zamani.

Beki huyo wa kati anasumbuliwa na majeraha ya goti ambapo kwa sasa anapambana ili arejee uwanjani baada ya kuumizwa na nyota wa Everton, Jordan Pickford kwenye Merseyside dabi mwezi uliopita.

Baada ya kufanyiwa vipimo na upasuaji Van Dijk taarifa zinaeleza kuwa ameanza kufanya mazoezi mepesi ambayo yatamfanya aweze kurejea kwenye kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England chini ya Jurgen Klopp.

Taarifa kutoka Liverpool imeeleza kuwa beki huyo anaendelea vizuri na upasuaji wake ulikwenda vizuri jambo ambalo limemfurahisha Klopp ambaye amesema kuwa wanatarajia kuwa na habari njema hivi karibuni.

Liverpool inapambana kutetea taji la ligi ikiwa inawakosa nyota wake wengi ambao ni mabeki ikiwa ni pamoja na Joe Gomez, Fabinho ambao wanasumbuliwa na majeraha.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

 

24 Komentara

    Habari nzuri kwasisi mashabiki

    Jibu

    Habari nzuri kwa Liverpool

    Jibu

    Habar njema sana

    Jibu

    habari njema kwa mashabiki wa liverpool

    Jibu

    kidogo mashabiki wa liverpool wameanza kuwa na matumaini mapya

    Jibu

    Good

    Jibu

    Ni habari njema kwa Liverpool

    Jibu

    Ni habar njema kwa cc mashabiki

    Jibu

    Ni vizuri wangempa nafasi ya kupunzika hili kuimarisha afya yake

    Jibu

    Habari njema hizi kwa mashabiki wa Liverpool wanaujua moto wake hats Chelsea walitaka kumsajili kwenye dirisha lililopita ila kwa bahati mbaya hawakufanya hivyo mana wanajua ujemedari wake

    Jibu

    Mwenye liver yake anarud

    Jibu

    Afadhal jamani

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Kaza kamba kijana

    Jibu

    Kila LA kheri

    Jibu

    Gud

    Jibu

    Gud

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Get well soon

    Jibu

    Itakua poa sana akirudi mchezoni

    Jibu

    Kazi nzuri inayopendeza

    Jibu

    Good

    Jibu

    Ni jambo jema sana kwetu mashabiki wake.

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe