Vita ya Kubaki EPL Yapamba Moto.

Ligi Kuu UingerezaEPL yazidi kupamba moto kwa vilabu vinavyopambana kuendelea kubaki kwenye ligi hiyo msimu ujao.

Baada ya kipigo cha Watford kutoka kwa Manchester City na Aston Villa kumchakaza Arsenal, timu hizi zinakuwa sawa kwa pointi wakiwa na tofauti ndogo ya magoli ya kufungwa na kufunga. Aston Villa wamepanda kwa nafasi moja wakiwa nafasi ya 17 wakati Watford wanashika nafasi ya 18.

Goli la Trezeguet katika kipindi cha kwanza lilitosha kupeleka matumaini ya kusalia kwenye EPL kwa mashabiki wa timu ya Aston Villa na kuwatoa katika nafasi ya kushuka daraja ambayo waliishikilia tangu tarehe 28 mwezi Februari, 2020.

Upande wa pili, Westham United wakiwa katika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa EPL watakutana na Manchester United leo ale Old Trafford. Woganga nyundo hawa wa London wanahitaji pointi 1 tu kujiweka katika nafasi nzuri ya kusalia kwenye ligi kuu msimu ujao wakiwa na tofauti kubwa ya magoli kati yao na Aston Villa, Watford na Bournemouth.

Kocha wa Aston Villa alisema ” Tuliwaona Watford wakicheza mapema na kufungwa. Tulijua tunahitaji ushindi ili angalau tuwafikie. Kwa ushindi huu, hatima ya kusalia ligi kuu ipo mikononi kwetu”

Kwa kipigo hiki kwa Arsenal, ni dhahiri kwamba kikosi cha Mikel Arteta hakiwezi kumaliza katika nafasi 6 za juu kwenye msimamo wa ligi kuu msimu huu. Hii ni mara ya kwanza kwa miaka 25.

Siku ya jumapili itakuwa ndio siku ya kujua mbivu na mbichi katika kumaliza msimu huu wa Ligi Kuu Uingereza. Aston Villa atakutana na Westham United, Arsenal uso kwa uso na Watford wakati Everton atamenyana na Bournemouth. Nani anashuka na nani anasalia Ligi Kuu?

 


Kwa sababu ya thamani ya pesa yako, kwa kila muamala unaofanya wa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Meridianbet unapata 5% bonasi.

SOMA ZAIDI 💰

43 Komentara

    Bonge la makala

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Kwel ni vita ambayo havijulikani nani atashinda

    Jibu

    Hebu tuone nani mshind maana ss mashabiki yetu macho#meridianbettz

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    United Nina Imani anaweza kushindwa mechi ya Leo maana sizani kama atakuwa tayari kupoteza nafasi

    Jibu

    Itakua mtanange wa kukata na shoka

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Hii ni nivutanikuvute#meridianbett

    Jibu

    kwa kweli ngoma ngumu

    Jibu

    Makala nzur

    Jibu

    Klabu nne za chini zitapambana ipasavyo ili visiweze kushuka daraja isipokua Norwich ambao wameshahakikiwa kushuka daraja,Aston Villa,Watford,Bournemouth mmojawapo ananafasi ya kusalia ligi kuu ingawa nafasi kubwa ipo kwa Aston Villa na Watford hivyo basi mechi za jumapili zitakua za kukata na shoka.

    Jibu

    Man u hawawezi kukubali kupoteza mechi ya leo maana kumekuwa na mvutano wa kupanda daraja

    Jibu

    Makala mazur

    Jibu

    hiyo kweli ni vita ambapo majibu yake ni kitendawili

    Jibu

    Hii kitu ndio tuliokuwa tunapenda kuiona kuwa aston villa apambane na kubaki EPL ila anatakiwa kukazaa butii ili kufanya vizuri ili kuendelea kusalia EPL

    Jibu

    Mechi hii
    Tusubiri matokeo

    Jibu

    Ama kweli.ni vita ya sintofaham kuwa nani atashinda

    Jibu

    Nasubiriaa kushuhudia kwa hamu

    Jibu

    Makala safi sana hii

    Jibu

    Mwisho was mechi kitaeleweka tuu

    Jibu

    Wiki ya kuona matokeo ya kushangaza katika mechi za Aston Villa, Westham and Watford. Kila inayokutana na timu hizi itarajie mchezo mgumu#meridianbettz

    Jibu

    Nasubili kuona nn kitatokea ndani ya dk 90

    Jibu

    Kwa mtazamo wangu Mimi naona Aston villa watabaki EPL bila Shaka kabisa

    Jibu

    Nice

    Jibu

    asante kwa makala

    Jibu

    Ni wakati wa makocha kuumiza vichwa kwani kila mmoja wao anataka kusalia kwenye ligi kuu hapo msimu kesho.

    Jibu

    Villa bado wana nafasi ya kubaki epl washinde mech zilizobaki

    Jibu

    Good news

    Jibu

    katika mechi za Aston Villa, Westham and Watford. Kila inayokutana na timu hizi itarajie mchezo mgumu#meridianbettz

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Habari njema Sana

    Jibu

    Tunasubir tuone

    Jibu

    Itakuwa bonge la mechi maana wote wakali

    Jibu

    Mechi za mwish zitaamua

    Jibu

    Hili balaa

    Jibu

    Ahsant kwa taarifa

    Jibu

    Hii ndo hiyo ilikuwa inahitajika kufahamika,na ni habari njema

    Jibu

    Aston villa anabaki aisee

    Jibu

    Nice#Meridianbettz

    Jibu

    Napata mashaka kwa Aston Villa kubaki ligi kuu

    Jibu

    Mtanange watari ulikuwa

    Jibu

    Tusubili tuone nani atashuka.

    Jibu

Acha ujumbe