Wabelgiji Waliowakilisha Vyema Premier League

Kuna wengi sana! Je, ni Lukaku? Hazard? De Bruyne? Dembele?

Subiri kwanza…

Angalia takwimu zao kisha tuambie kati ya mastaa hawa wa Ubelgiji na upige kura kutuambia ni nani anayestahili kuwa mfalme wa taifa lao akiwakilisha vyema Ligi Kuu ya Uingereza.

Nako Ubelgiji kuna vipaji vikubwa sana na wamekuwa wakifanya vyema sana pale Premier League, hatuwaachi hivi hivi, tunawapongeza sana na kuwasifu mno hawa wachezaji.

Twende zetu Ubelgiji…

Katika muda wa muongo mmoja uliopita wachezaji wa Ubelgiji wamekuwa bora sana na kufanya vyema mno hasa kwenye Premier League.

Tangu pale Philippe Albert alipokuwa ndiye mchezaji wa kwanza kushiriki mashindano hayo mwezi wa Agosti mwaka 1994 wakati alipoingia kuichezea klabu ya soka ya Newcastle United, baadaye wengine wapatao 56 walijiunga katika michuano hiyo.

Kati ya hao wote aliyefanikiwa sana ni Eden Hazard. Alishinda tuzo ya EA SPORTS Player of the Season msimu wa mwaka 2014/15 katika mbio zake mojawapo kati ya zile mbili alizotwaa taji akiwa na mabingwa wa Chelsea.

Magoli yake dhidi ya klabu ya soka ya Arsenal msimu wa 2016/17 akiwa na West Ham United msimu wa mwaka 2018/19 na akashinda tuzo za Budweiser Goal of the Month wakati pia akiwa anawania zawadi ya Cadbury Playmaker kwa kutoa assists nyingi zaidi katika msimu wa mwisho kwake ndani ya Premier League.

Thibaut Courtois alikuwa ni mwenzake na Hazard na akashinda tuzo ya Golden Glove msimu wa mwaka 2016/17 akifanikiwa kuwa na jumla ya clean sheets 16.

Naye Romelu Lukaku alianza mishe mishe zake kule kwenye michuano ya soka ya PL akiwa na klabu ya The Blues na akafanikiwa kujiweka vyema kabisa akiwa pale Everton, ikafuatiwa na mafanikio makubwa alipokuwa kwa mkopo kule West Bromwich Albion, kabla hajajiunga na Manchester United msimu wa mwaka 2017.

Mshambuliaji huyo ndiye Mbelgiji pekee kufanikiwa kufikia idadi ya magoli 100 katika mashindano hayo ya Uingereza.

Anayefunika wote wa kutoka taifa la Ubelgiji ni mchezaji Vincent Kompany, ambaye ana medali nyingi zaidi za PL ukilinganisha na wenzake wa taifa moja, ameshinda medali zote nne akiwa kama kepteni wa klabu ya soka ya Manchester City.

Beki huyo wa kati alikuwa ni mtu muhimu sana alipokuwa pale Etihad Stadium, alishambilia na kuachia shuti kali sana walipocheza dhidi ya klabu ya Leicester City mwezi Mei mwaka 2019 wakati alipokuwa katika hekaheka za kuwania taji lake la hivi karibuni ambapo walishinda.

Mchezaji huyu Kompany alijiunga klabuni kwa Man City akiwa na mwenzake kutoka taifa moja, Kevin De Bruyne mwaka 2015.
De Bruyne anaongoza kwa Wabelgiji wote kwa kutoa assists nyingi zaidi.

Assists zake kumi na sita kati ya zile 62 zilipatikana msimu wa mwaka 2017/18 wakati aliposhinda tuzo kubwa ya Playmaker of the Season inayotolewa kila mwaka.

Takwimu zinazoongoza kutoka kwa Wabelgiji ndani ya PL

MechiMagoliAssists
Vincent Kompany265Romelu Lukaku113Kevin De Bruyne62
Marouane Fellaini260Eden Hazard85Eden Hazard54
Romelu Lukaku252Christian Benteke71Romelu Lukaku35
Eden Hazard245Marouane Fellaini37Christian Benteke20
Simon Mignolet245Kevin De Bruyne31Kevin Mirallas20

Katika misimu ya hivi karibuni wachezaji watatu kutoka Ubelgiji wamefanya mambo makubwa sana kwa klabu ya soka ya Tottenham Hotspur.

Mchezaji wa taifa hilo aliyepewa unahodha mara nyingi zaidi, Jan Vertonghen, alijibiidisha sana na kuwa moja kati ya walinzi wa kati wanaoongoza klabuni pale kwenye ligi ya Premier League na ametajwa mara mbili kuwa ni mshindi wa tuzo ya PFA Team of the Year.

Vertonghen alijiunga na klabu ya soka ya Spurs pamoja na Toby Alderweireld mwaka 2015 na kama ilivyokuwa kwa beki mwenzake wa kati, alichaguliwa kuwania tuzo ya PFA Team of the Year katika mismu wake wa kwanza klabuni pale.

Wote hao, pamoja na Mousa Dembele ambao wanakipiga katika nafasi muhimu sana uwanjani, walikuwa ni watu muhimu sana katika mafanikio ya klabu ya soka ya Spurs ambapo waliruhusu magoli 26 pekee katika msimu wa mwaka 2016/17 na wakaweka rekodi ya kumaliza msimu wakiwa katika nafasi ya pili msimu huo.

Unaweza kuangalia mabao bomba yaliyofungwa na wachezaji wa Ubelgiji na kutazama takwimu hizo hapo juu kisha ukapigia kura mchezaji unayeamini anastahili kuwa ndiye mfalme wa Ubelgiji aliyecheza ndani ya ligi ya Premier League.

Sema neno hapo.

Unadhani ni nani anastahili kuwa mfalme wa Ubelgiji?
• Toby Alderweireld
• Thibaut Courtois
• Kevin De Bruyne
• Mousa Dembele
• Eden Hazard
• Vincent Kompany
• Romelu Lukaku
• Jan Vertonghen

44 Komentara

    Historia yao na mchango wao n mkubwa sana

    Jibu

    Historian yao na mchango wao ni mkubwa sana

    Jibu

    Wengi wamefanya kazi nzuri sana

    Jibu

    walikuwa vzr mno waliiwakilisha ipasavyo

    Jibu

    Ahsante meridian kwa habari nzuri#merisianbettz

    Jibu

    Walikiwa wana mchango mkubwa

    Jibu

    Namkubali Sana edin hazard

    Jibu

    Eden hazard#meridianbettZ

    Jibu

    Romelu Lukaku huyo ndiye Mbelgiji pekee kufanikiwa kufikia idadi ya magoli 100 katika mashindano hayo ya Uingereza#meridianbettz

    Jibu

    Those guys are the best

    Jibu

    Wengi wao wamawajika ipasavyo

    Jibu

    Wote wako sawa mana wamewajibika wapasavyo

    Jibu

    Nawapongeza sana na kuwasifu mno hawa wachezaji mana Kila mmoja aliweza kufanya vizuri ktk nafasi yake

    Jibu

    Wote wanajitahidi kiukweli.

    Jibu

    Wote wamefanya kazi safi kabisa

    Jibu

    Wengi wame fanya kazi nzuri

    Jibu

    Wote walifanya vzr lkn lukaku the best

    Jibu

    Wengi wamewajibika kiukweli

    Jibu

    Mie naona niwasifie wote kwa ujumla wako vzr

    Jibu

    De bruyne yupo vizuri na bado ana muda wa kufanya makubwa zaidi

    Jibu

    edin hazard yuko vizuri

    Jibu

    Wote wanaistori na nchi yao..!

    Jibu

    kila mmoja aliwajibika kwa nafasi yake, kutokana na position na timu aliyopo

    Jibu

    gud newz asante

    Jibu

    Waliwajibika ipasavyo👏👏

    Jibu

    Kila mtu and historia yake katika soka

    Jibu

    Kwangu Hazard Eden

    Jibu

    hazard alikuwa wa moto

    Jibu

    Asante kwa makala#meridianbettz

    Jibu

    Wote wamefanya kazi nzuri

    Jibu

    Ubelgiji kuna vipaji

    Jibu

    Namkubali Thibaut Courtois #Meridianbettz

    Jibu

    Wametisha sana

    Jibu

    Wako vizur Sana

    Jibu

    Hazard kiboko mwe

    Jibu

    De Bruyne na Hazard ni moto sana

    Jibu

    Meridianbet kwa taarifa mko vizur sana

    Jibu

    Walifanya vizur sana hao majamaa

    Jibu

    kwa upande wangu Vincet Kompany

    Jibu

    Eden Hazard was the best EPL from Belgium#meridianbettz

    Jibu

    Welcome back to the Premier League we missed you

    Jibu

    Kwangu mimi Dembele yuko vizuri sana

    Jibu

    Kompany is agreat

    Jibu

    Wako vizur sana

    Jibu

Acha ujumbe