Wachezaji Stuart Armstrong, Kieran Tierney na Ryan Christie wa timu ya taifa ya Scotland watakosa nusu-fainali ya mchujo wa kufuzu kwa fainali za Euro 2021 dhidi ya Israel kwa sababu ya Covid-19.
Japo Armstrong ndiye wa pekee aliyepatikana na virusi vya corona, Tierney ambaye ni beki wa Arsenal na Christie wa Celtic watalazimika kujitenga kwa siku 14 zijazo kwa kuwa walikuwa na Armstrong pamoja mazoezini.
Wachezaji hao hawatakuwa pia sehemu ya kikosi cha Scotland kitakachoshiriki mechi za Nations League dhidi ya Slovakia na Jamhuri ya Czech.
Christie atakosa pia mechi itakayowakutanisha Celtic na Rangers mnamo Oktoba 17, 2020 huku Tierney akitarajiwa kukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) litakalowakutanisha na Manchester City siku hiyo hiyo.
Armstrong ambaye ni kiungo wa Southampton, hakupatikana na virusi vya corona alipowasili katika kambi ya Scotland mnamo Oktoba 5, 2020.
Hata hivyo, vipimo vya afya vilivyofanywa na Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa) vilibainisha kwamba mchezaji huyo alikuwa anaugua Covid-19 na hivyo atajitenga kwa siku 10 kuanzia Oktoba 6, 2020.
“Ingawa hizi ni taarifa za kuvunja moyo, muhimu zaidi ni kuzingatia kanuni zilizopo za afya na kuhakikisha kwamba wachezaji wengine wanasalia katika hali nzuri,” akasema kocha wa Scotland, Steve Clarke.
Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!
Rehema
Duuuh hii ni hatari
Sauda
Corona noma
Angelina
Covid19 bado ni tishio kwa wenzetu wazid kuchukua tahadhari
Tatu
Wanatakiwa wawe makini na hili janga
Theckla
Pole yao
Adelta
Hili gojwa Ni hatari sana wanatakiwa waendelee kujikinga pole yao
magdalena
huu ugonjwa unazidi kuleta gumzo kali sana jamani
Fatina mfingi
Umakin unaitajika san dhid ya ili janga
Dorophina
Huu ugonjwa unaendelea kuwa tishio kubwa nchi za wenzetu
Lydia Emmanuel Magoti
Duu pole yao
Caroline
Sad newz
aisha
Poleni sana duuh covid 19 ni hatari sana
Mwajumah
Duuh pole yao
Mwanahamisi
Pole yao
Elika
Pole sana kwao..huu ugonjwa sio poa
Devotha
Pole yao
Nasra
Pole yao
Venerose
Huu ugonjwa bado no janga la dunia
Amiri Kayera
Corona inakatsh San shughur za michez
Neema
Pole yao
Saupha mohamed
Corona sio poa
Fatuma kasomo
Pole yao
Sabrina
Duuh waugue pole
Theonestina
Pole yao
Gabriel
Habar ya kusikitisha sana
felister
duh wajifushe nyungu kama vipi
Rose kapinga
Pengo kubwa
Samiah
Duuuh
Janeflora malisa
Pole maan hapo ni mtian mkbwa
Ernest
Corona sio pouwa
Tahiya
Duuh atarii sana
Issa
Covid 19 ni balaa lingine
Hopemwaikuka
Dah! So sad
Povel
Duh majanga kwl
David Pere
Wachezaji hao hawatakuwa pia sehemu ya kikosi cha Scotland kitakachoshiriki mechi za Nations League dhidi ya Slovakia na Jamhuri ya Czech.