KOCHA Mkuu wa Azam FC, Abdihamid Moallin ameonyeshwa kuridhishwa na viwango vya wachezaji wake licha ya kupoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Wadi Degla (0-1).

Mchezo huo ulipigwa jana jumatano nchini Misri ambapo Azam wameweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao ambao unatarajiwa kuanza Agosti 17 mwaka huu.

Akizungumzia hilo, Moallin alifunguka kuwa “Tunashukuru mchezo umemalizika salama, sasa nimeanza kupata picha halisi ya kikosi changu.

“Matokeo hayakuwa muhimu sana kwa upande wetu bali nilitamani kuona jinsi gani wachezaji walishika kile ambacho nimewafundisha kwa muda mchache ambao tumeanza mazoezi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa