Vigezo vifuatavyo vimetumika kulinganisha ubora wa wachezaji hawa katika msimu wa 2020/21 tu:
-Magoli yaliyofungwa
-Magoli katika kila mchezo
-Magoli ndani ya dakika 90
-Mchango wao kwa ujumla (usaidizi wa magoli)
1. Robert Lewandowski (Bayern Munich)
Kwa sasa ndiye mchezaji bora zaidi duniani na ndio sababu anaongoza orodha hii ya washambuliaji 10 bora duniani.
Ameshiriki mechi 47
Amefunga magoli 53
Ametoa usaidizi wa magoli 9
Amefunga magoli 1.28 kwa kila mechi
Amefunga magoli 1.35 kwa kila dakika 90
Robert Lewandowski ambaye ni mshambuliaji wa Poland ameiongoza Bayern Munich kunyakua taji la Bundesliga baada ya kufunga mabao 53 katika mechi 47.
2. Harry Kane (Tottenham Hotspur)
Mshambuliaji huyu wa Tottenham ameshikilia nafasi hii kwa muda mrefu katika historia ya kandanda. Ameisaidia klabu yake kumaliza Ligi Kuu ya Premia katika nafasi ya kuheshimika baada ya kufunga mabao 30 na kusaidia ufungaji wa mabao 18.
Ameshiriki mechi 54
Amefunga magoli 30
Ametoa usaidizi wa magoli 18
Amefunga magoli 0.55 kwa kila mechi
Amefunga magoli 0.67 kwa kila dakika 90
3. Erling Haaland (Borussia Dortmund)
Erling Haaland ambaye ni mchezaji nyota na raia wa Norway amekuwa akisakwa na karibu klabu zote kubwa.
Haaland, akiendelea kujiimarisha anapigiwa upatu kuwa mmoja wa washambuliaji mahahiri duniani.
Ameshirika Mechi 52 msimu huu
Amefanikiwa kufunga mabao 49
Alitoa usaidizi wa magoli 9
Alifunga magoli 0.94 kwa kila mechi
Alifunga magoli 1.2 kwa kila dakika 90
4. Romelu Lukaku (Inter Milan)
Inter Milan kwa mara ya kwanza wameshinda taji la Serie A ndani ya miaka 11.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji alifunga mabao 23 katika msimu wake wa kwanza nchini Italia. Ushirikiano wake na Lautaro Martinez, umeisaidia sana klabu yake kupata ufanisi.
Ameshiriki mechi 53
Alifunga magoli 39
Ametoa usaidizi wa magoli 12
Alifunga magoli 0.71 kwa mechi
Alifunga magoli 0.87 kwa kila dakika 90
5. Luis Suarez (Atletico Madrid)
Barcelona ilimuuza Luis Suarez kwa Atletico Madrid kwasababu ilihisi kiwango cha uchezaji wake kimeshuka lakini nyota huyo anasalia kuwa kiungo muhimu kwa Atletico Madrid kushinda taji la La Liga.
Ameshiriki mechi 38
Alifunga magoli 21
Alitoa usaidizi wa magoli 3
Alifunga magoli 0.55 kwa kila mechi
Alifunga magoli kwa kila dakika 90
6. Cristiano Ronaldo (Juventus)
Cristiano Ronaldo ni mmoja ya washambuliaji hodari zaidi duniani. Gumzo limeibuka kuhusu kushuka kwa kiwango cha mchezo wake lakini hata hivyo amefunga mabao 41 katika mechi 55 za msimu wa 2020/21.
Ameshiriki katika mechi 55
Alifunga magoli 41
Alitoa usaidizi wa mabao 5
Alifunga magoli 0.75 kwa kila mechi
Alifunga magoli 1.15 kwa kila dakika 90
7. Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain)
Kasi na uwezo wake kuchenga umempatia Kylian Mbappe aliye na umri wa miaka 22 sifa na kuwatia imetia kiwewe walinzi wa timu zote duniani.
Alicheza mechi 58
Alicheka na wavu mara 48
Alitoa usaidizi wa magoli 11
Alifunga mabao 0.83 katika kila mechi
Alifunga mabao 1.15 ndani ya dakika 90
8. Karim Benzema (Real Madrid)
Karim Benzema amekuwa kiungo muhimu katika safu ya mashambulizi ya Real Madrid tangu Cristiano Ronaldo alipoondoka
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa aliiongoza Real Madrid kushika nafasi ya pili katika La Liga.
Ameshiriki katika mechi 45
Akafanikiwa kucheka na wavu mara 30
Alitoa usaidizi wa magoli 9
Alifunga magoli 0.66 katika kila mchezo
Alifunga mabao 0.72 ndani ya dakika 90
9. Ciro Immobile (Lazio)
Mchezaji wa timu ya Lazio alionyesha ubora wa kufumania nyavu katika Msimu 2020/21:
Amecheza mechi 47
Alifanikiwa kufunga magoli 27
Alitoa usaidizi wa magoli 8
Alifunga mabao 0.57 katika kila mchezo
Alifunga mabao 0.66 ndani ya dakika 90
UEFA Champions League.
10. Andre Silva (Eintracht Frankfurt)
Baada ya msimu mbaya akiichezea AC Milan, Kiungo huyo wa Ureno amekuwa makini sana msimu huu.
Mshambuliaji huyo ameifungia Frankfurt mabao 28 na kusaidia ufungaji wa mabao 5 katika mechi 32 za ligi msimu huu
Alicheza mechi 34
Alifunga magoli 30
Alisaidia katika ufungajiwa mabao 5
Alifunga mabao 0.88 katika kila mechi
Alifunga magoli 0.94 ndani ya dakika 90
MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
magdalena
Wamefanya kazi nzuri