Waingereza Wana Wafubaza Makinda Wao Kwa Majukumu

Waingereza wamefanya hiikua kama utamaduni kwa kuwatumia vibaya vijana wao wanao chipukia na kuonekana wana kasi . Niliwahi kupiga stori na Mshikaji wangu mmoja yupo England ni Mtaalam wa tiba za Wachezaji katika mazungumzo yetu tuligusia afya za Wachezaji vijana England

Nilimuuliza kwanini Makinda wengi England wanapotea kabla ya kufika miaka 27 ambayo ni prime age ya football?

Majibu yake yalikuwa;

Watoto wengi wanaanza kubeba mzigo mkubwa ingali wadogo, nikupe mfano wa Marcus Rashford, tangu LVG amlete kwenye game hajapumzika tena sio klabu wala National team

Unafahamu kuwa Rash anacheza akiwa na majeraha wakati mwingine? Hii ni kutokana na Waingereza wanajua umuhimu wake kikosini, mpaka sasa anasumbuliwa na mgongo ila bado anacheza mpira na hajapumzishwa

Kinachowaumiza ni majeraha na hawapati muda wa kupumzika, tofauti na nchi zingine, ambapo vipaji vyao wana mikakati ya kuvilinda, mfano Ujerumani kuita wachezaji national team wanafanya rotation

Ujerumani licha ya ubora wa Sane ila walimtema kuelekea Wordl Cup wakamwambia bado ana muda wa kupumzika na nafasi yake ipo kutokana na umri, hii ni tofauti sana na waingereza.

Jack Wilshere unamkumbuka? Yupo wapi sasa, story ilikuwa ni hayo hayo majeraha.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe