Kura yako kwa nani hasa? Je, ni Ozil? Klinsmann? Au Sane? Hebu jichagulie mchezaji wako aliyetisha zaidi akiwa mwanasoka wa Ligi Kuu ya Uingereza akitokea taifa kubwa la Ujerumani.
Lakini, hebu kwanza, kabla hatujafika huko tuangalie takwimu za wachezaji wa taifa hilo tukihusisha na ushiriki wao kwenye Premier League.
Kwa sasa tunasherehekea mafanikio yao waliyoyapata wakiwa na klabu za Uingereza katika nyakati mbalimbali. Wamekuwa na vipaji vya hali ya juu sana. Na tungependa mno kujua mtazamo wako wa nani ni mkali kati yao.
Kumekuwa na jumla ya wanasoka 69 waliocheza ndani ya Premier League tangu pale Matthias Breitkreutz alipotokea benchi akiichezea klabu ya soka ya Aston Villa waliokuwa wakicheza dhidi ya Manchester City mnamo mwezi Desemba mwaka 1992.
Uwe Rosler alikuwa ni Mjerumani wa kwanza kufunga bao katika michuano hiyo wakati alipoifungia timu ya soka ya Man City mwezi Machi mwaka 1994.
Miezi michache tu baadaye naye Jurgen Klinsmann akajiunga na klabu ya Tottenham Hotspur na kufanikiwa kufanya makubwa sana wakiwa pamoja pale alipofunga bao katika gemu yake ya kwanza na kusaidia sana katika ushindi mnono wa magoli 4-3 wakiwa pale kwa Sheffield Wednesday.
Ukitazama takwimu za assists, anayekamatia kilele cha wote miongoni mwao, kwa hakika ni Mesut Ozil akiwa ametoa jumla ya pasi 54 za magoli.
Kumi na tisa kati yake alizifikia katika msimu mmoja wa ligi, mwaka 2015/16, na hapo anakuwa amezidiwa na mwanakabumbu Thierry Henry, ambaye alifikisha jumla ya magoli 20 katika msimu wa mwaka 2002/03.
Pia, Ozil anashikilia rekodi ya kuwa na magoli mengi zaidi yaliyofungwa na mchezaji kutokea taifa la Ujerumani katika michuano hiyo, anawazidi magoli manne akina Klinsmann pamoja na mwenzake Rosler.
Wachezaji wawili ambao walicheza nafasi ya mido wakafanya poa sana kwenye Premier League kabla ya ujio wa Ozil mwezi Septemba mwaka 2013 walikuwa ni Dietmar Hamann pamoja na Michael Ballack.
Hamann anakaa kwenye nafasi ya pili nyuma ya mwenzake Robert Huth katika orodha ya wachezaji walioingia uwanjani kwa muda wote kutokea Ujerumani, amecheza jumla ya mechi 268 akiwa na klabu za soka za Newcastle United, Liverpool pamoja na ile ya Man City.
Ballack alidumu katika klabu moja pekee katika mashindano hayo na kusaidia klabu ya soka ya Chelsea kushinda taji msimu wa mwaka 2009/10 akiwa na uzoefu na umaridadi mkubwa sana kwenye taaluma yake hiyo.
Takwimu zinazoongoza kutoka kwa wachezaji wa Ujerumani waliohudumu PL
Mechi | Magoli | Assists | |||
---|---|---|---|---|---|
Robert Huth | 322 | Mesut Ozil | 33 | Mesut Ozil | 54 |
Dietmar Hamann | 268 | Jurgen Klinsmann | 29 | Leroy Sane | 28 |
Mesut Ozil | 184 | Uwe Rosler | 29 | Dietmar Hamann | 22 |
Per Mertesacker | 156 | Leroy Sane | 25 | Christian Ziege | 18 |
Jens Lehmann | 148 | Robert Huth | 21 | Thomas Hitzlsperger | 17 |
Kwa miaka ya hivi karibuni, Wajerumani wawili wamefanya makubwa sana kwa kikosi cha meneja mkali Pep Guardiola pale Man City.
Ubora na umachachari wa mchezaji Leroy Sane uliifanikisha sana klabu ya City kutwaa taji katika kampeni zao za msimu wa mwaka 2017/18 na ule wa mwaka 2018/19, wakati ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alichangia upatikanaji wa mabao 25 na kutoa pasi 28 za magoli katika mechi 89 mpaka sasa.
Mchezaji mwingine, Ilkay Gundogan naye pia amekuwa mtu wa muhimu sana kwa kikosi hicho tangu awasili klabuni pale mnamo mwezi Juni mwaka 2016.
Kwenye takwimu za magoli, Jens Lehmann alitisha sana akiwa na Arsenal katika msimu wao wa “Invincible” mwaka 2003/04, pale alipoweka clean sheets 15 kwa ujumla wake.
Nafasi ni yako sasa kutazama takwimu hizo hapo juu na kuangalia mabao maridadi kabisa kutoka kwa Wajerumani waliohudumu ndani ya EPL kabla hujatuambia ni nani kati yao anastahili kuwa mfalme wao:
- Michael Ballack
- Ilkay Gundogan
- Dietmar Hamann
- Jurgen Klinsmann
- Jens Lehmann
- Mesut Ozil
- Leroy Sane
Hamidu
Sane talent player.# meridianbettz
Aziza mushi
Asanteni meridianbet kwa taarifa
frank patrick
Michael Ballack bonge la player alikiwasha sana Chelsea pale
Zeiyana iddi
Ozil hanajua mpira ila hajawai kuchukua taji
Theonestina
Asante meridianbet kwa kutujuza
Povel
Per mertesacker moja ya mlinzi Bora epl na ujerumani moja ya vitasa wangu na wakubal ni mtu wakaz sana mjerumani mashine thanks meridian kwa update
Gabriel
Ozil mtu mbaya
Evaluziga
Ozili Yuko juu bwana
Antony Luseno
German players uwa wapo vizuri sana popote watakapoenda wanakiwasha
Carolyne
Habari njema
Juliana
Asante meridianbet kwa taharifa
Shafii
Wamefanya makubwa sana hao watu EPL sio ligi ya kitoto hongera zao
Mwanaidi
Namkubali sana ozil
Swai
Hatari sana
Ernest
Gundogan moto wa kuotea mbali
sylvester
Jurgen Klinsmann ndio kwangu bora anaieshi #meridianbettz
Kenani
Noma sana hyu mtu
Rehema Dickson
Habari za michezo napata meridian na pesa pia napata kwel mko vizuri
SADICK
Kwangu mimi Michael Ballack alikuwa bora. Asante meridianbet kwa makala nzuri.
Christopher
Ballack alikuwa mtu hatari kipindi chake pale Stamford Bridge
Neema hassan
Ozil yuko vizuri#asante meridianbet kwa makala
Tatu
Meridian mpo vizuri
Emmy cleopa
Ozil anaweza
Asia Abdy
Mafundii
Neema juma
Mie namkubali ozil jamani
Isha
Ozil namkubali sana
Lombo
gud newz asante
Theckla
Kwa upande wangu ozil ni bora zaidi
felister
asanteni meridian kwa makala nzuri
Furahav
Ozil anatisha.
Salma
Ozil alitisha
farida ahmadi
Ozil mtu mbaya Yuko vzr hanajua Sana mpira