Chini ya utawala wa Wallace Karia ni muda sasa suala la maadili kwa watendaji na wadau wa soka limekuwa likizungumzwa sana kila mahali, na hii ni kutokana na kanuni zilizowekwa zinaonekana kuwa kali sana, kwa mfano kamati ya maadili iliposikiliza shauri la Haji Manara na Rais wa TFF Wallace Karia.

wallace karia, Wallace Karia: Ukishandana na Mamlaka Utaumia., Meridianbet

Kamati hiyo ya maadili ilibaini kuwa Manara kakiuka maadili na hivyo wakampa adhabu ya kumfungia kwa miaka 2 na faini ya Milioni 20. Leo nakupitisha kwenye adhabu za baadhi ya wadau wa mpira hapa nchini.

Mwaka 2013, kamati ya maadili ilimfungia miaka 20 mdau wa soka ndugu Richard Julius Rukambura, kujihusisha na mpira wa miguu.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by EastAfricaTV (EATV) (@eastafricatv)

Mwaka huo huo, katibu mkuu wa sasa wa TFF, Kidao Wilfred, wakati huo akiwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, alihukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni 1. Alitakiwa alipe ndani ya siku tatu la sivyo afungiwe mwaka mmoja…akalipa! Wakati huo TFF ilikuwa chini ya Rais Leodegar Tenga.

Mwaka 2014, kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilimfungia miaka 7, mdau wa soka, Dkt. Damas Ndumbaru, kukijisisha na mpira wa miguu. Wakati huo TFF ilikuwa chini ya Rais Jamal Malinzi.

wallace karia, Wallace Karia: Ukishandana na Mamlaka Utaumia., Meridianbet
Huko mtaani na mitandaoni kumekuwa na mitazamo tofauti juu ya anayetekeleza hizo kanuni ni taasisi au ni mtu anayeongoza hiyo taasisi, basi kimsingi taasisi inaongozwa kwa sheria na taratibu zake mtu anayekuwa ndani ya taasisi huwa chini ya kanuni na misingi ya taasisi hivyo mtu akikosea ataadhibiwa na taasisi na sio mtu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa