Wamepoteza Muelekeo!

Klabu ya Arsenal imepotea kabisa kwenye ramani mara baada ya kuwa na matokeo ambayo hayaridhishi kabisa kipindi cha karibuni ambacho kilipelekea hata kocha wake, Emery kuondoshwa klabuni hapo jambo ambalo lilitokana na aina ya matokeo ambayo klabu hiyo ilikuwa ikiyapata.

Huenda hata maamuzi ya kumuondosha kocha huyo yalikuwa ya haraka mno kwa sababu hata baada yake bado hakuna mabadiliko yanayoonekana ndani ya klabu hiyo. Wamekuwa ni timu inayopoteza mechi rahisi ambazo kwa hali ya kawaida ni mechi za ushindi kwa klabu kama Arsenal.

Kiuhalisia kwa sasa wamepoteza kabisa mwelekeo na wanapaswa kurejea nyuma kabisa kuanza kutathmini juu ya nini wakifanye ili kurejea kwenye ubora wao. Hii ni kuanzia usajili wa nyota wao hadi kipande cha mwisho kabisa cha hali ya maelewano baina ya uongozi na nyota wao wanaowakilisha klabu.

Wana jukumu kubwa sana la kuwaaminisha mashabiki wao kwamba kile wanachokifanya ni mapito ila watarejea upya baada ya usajili kwa sababu hadi sasa klabu hiyo imepoteza kabisa hadhi yake mbele ya mashabiki ambao walikuwa wanaiamini klabu hiyo.

Hata baada ya ujio wa Emery kama klabu walikuwa wanaamini kwamba klabu hiyo imerudi kwa ajili ya kusaka nafasi za ushiriki wa makombe makubwa lakini hadi sasa tatizo limesalia pale pale ambapo kama klabu watapaswa kubaki wakisubiri dirisha la usajili kufunguliwa ili kuongeza nguvu kikosini hapo.

Yaliyojiri jana

Jana wamepata kipigo mbele ya Brighton and Hove Albion katika matokeo ambayo yaliwashangaza wengi. Ilionekana kuwa ni mechi ya wazi kwa Arsenal lakini manbo hayakwenda hivyo, ikawa ni tofauti kabisa na mategemeo yao. Hali hiyo kwa hakika ilionekana kama kitu ambacho siyo cha kawaida kwa kikosi hicho.

Hadi sasa hawana kocha ambaye angeanza kufikiri juu ya mbadala wa wachezaji ambao anapaswa kuwa nao kikosini hapo lakini kama kocha msaidizi ana kubwa la kufikiri kwa namna gani anaweza kuwa na mbadala wa kufanya vyema. Kocha msaidizi aliyepewa nafasi hiyo ana kila linalowezekana kupata matokeo na kuwajengea imani mashabiki.

2 Komentara

    Hawako vizuri sana.

    Jibu

    Kwl hawapo vzr sana

    Jibu

Acha ujumbe