Beki wa kulia wa klabu ya Manchester United Aaron Wan Bissaka anahitaji na timu ya taifa ya Congo kwajili ya kuiwakilisha katika michuano ya kimataifa nchi hiyo.
Shirikisho la soka nchini Congo linaelezwa kutuma maomba kwa beki Aaron Wan Bissaka ili awakilishe nchi hiyo, Lakini mpaka sasa hakuna maamuzi yeyote ambayo yamefanywa kwa upande wa mchezaji huyo.Beki huyo wa kulia wa Manchester United amezaliwa na kukua nchini Uingereza lakini asili yake ni Congo, Hivo shirikisho la soka nchini Congo limeona liwasiliane na mchezaji huyo ili awawakilishe taifa la asili yake.
Shirikisho la soka nchini Congo limeshawishika na kumshawishi beki huyo kujiunga nao kutokana na beki huyo kutoitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza, Hivo shirikisho hilo likaona linaweza kumshawishi arudi nyumbani.Beki Aaron Wan Bissaka mpaka sasa hajatoa majibu kwa shirikisho la soka nchini Congo juu ya kuanza kulitumikia taifa hilo la asili yake, Lakini kama mchezaji huyo atakubali kuitumikia Congo ni wazi atakua nje ya klabu hiyo kuanzia Januari 13 mpaka Febuari 11.