Kiungo wa zamani wa klabu ya Southampton ambaye anakipiga klabu ya Westham kwasasa James Ward Prowse ameanza vizuri kwenye klabu hiyo ambapo sasa kahusika kwenye mabao matatu ndani ya timu hiyo.
Kiungo wa Ward Prowse ameonesha kuingia kwenye mfumo wa klabu ya Westham mapema chini ya kocha David Moyes, Kwani namba zake ndani ya timu hiyo kwenye michezo mitatu ambayo ameshacheza kwenye klabu hiyo.Klabu ya Westham walifanikiwa kushinda ugenini katika mchezo walioifunga klabu ya Brighton kwa mabao mawili kwa moja, Huku kiungo huyo alifanikiwa kufunga bao jana kati ya magoli matatu yaliyofungwa jana.
Katika mchezo wa jana ambao Westham wameshinda kwa mabao matatu dhidi ya Bighton uliwapeleka mpaka nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya michezo na kufikisha alama saba ambapo hawajapoteza mchezo mpaka sasa.Kiungo Ward Prowse alifanikiw akufunga jana lakini katika mchezo uliomalizika dhidi ya Chelsea ambapo walishinda mabao matatu kwa moja tena ambapo kiungo huyo alipiga pasi mbili za mabao na jana alipofanikiwa kufunga bao moja anakua amehusika kwenye mabao matatu na hii inaonesha mchezaji huyo ameanza vizuri klabuni hapo.