Washambuliaji Mwiba Uingereza

Baada ya Manchester City kunyanyua ndoo ya ubingwa ikiwa ni alama ambazo nafasi yake ni ndogo sana kiutofauti na klabu ya Liverpool; basi kuna aina ya wachezaji ambao kwa hakika wameweza kuonesha thamani yao mbele ya walinzi na walinda mlango kwa namna ambayo ni ya pekee sana kutokana na ufundi wao.

Kitu kinachomjenga mshambuliaji na kumuona anafaa ni ile nafasi yake ya kucheza kwenye nafasi ambayo anakutana sana na walinzi wa klabu anayocheza nayo. Ligi ya Uingereza kwa msimu huu imeweza kuonesha upekee wa aina yake hasa katika nafasi hiyo ya washambuliaji walioweka maajabu makubwa ambayo. Kuna watu kama;

Pierre-Emerick Aubameyang, ni miongoni mwa wachezaji ambao Wenger aliweza kuwashusha kikosini hapo. Kwa hakika ameweza kuacha mazingira salama na alifanya chaguo sahihi ambalo matunda yake yameonekana kwa nafasi kubwa sana. Kubwa lililomfanya aweze kufanya vizuri pamoja na kupata ugumu wakati wa kuanza kuizoea ligi hiyo ni jambo pia ambalo lilimchelewesha sana kuanza kufunga na kwa hakika ameweza kuwaongoza wenyeji wengi hadi sasa ndani ya ligi.

Sergio Aguero, ni washambuliaji wanaojua kufunga na wapi goli lipo. Amekuwa msaada mkubwa kuelekea kutwaa taji hilo la ligi kwa klabu yake ya Manchester City. Nafasi yake ameweza kuitumia ipasavyo na ni sahihi pia kuweza kukaa katika nafasi hiyo kitokana na ufundi wake. Ameweza kumaliza ligi akiwa na magoli 21 nyuma ya wafungaji watatu ambao waliweza kumzidi goli moja pekee.

Alexandre Lacazette, wameweza kuendana kasi na kulandana kimfumo na Pierre kwa kiwango kikubwa sana. Mchezaji huyu amekuwa msaada mkubwa kuchagiza magoli mengi ambayo yameweza kufungwa na mshambuliaji mwenzake licha ya yeye pia kuwa na magoli ya kutosha. Ni aina ya washambuliaji ambao wameweza kuwa na msimu imara sana pamoja na kwamba timu haijaweza kukaa katika nafasi yoyote ile ndani ya ligi.

Raul Jimenez, mshambuliaji hatari wa klabu ya Wolves na raia wa Mexico ambaye amekuwa mwiba sana ndani ya kikosi chake hicho. Ameweza kuwanyanyasa vigogo wengi sana msimu huu akiwa na timu yake ambayo haina muda mwingi ndani ya ligi. Kwa hakika ni aina ya washambuliaji ambao klabu nyingi zinaweza kutamani kuwa nao.

Son Heung-Min, kwa nafasi kubwa ameweza kuziba ule upenyo wa kumkosa Kane ndani ya kikosi chao. Ameweza kugeuka mchezaji muhimu sana na mwenye msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji baada ya kuweza kuifikisha timu yake kwenye nafasi nzuri ndani ya michuano mingi mikubwa inayochezwa barani Ulaya.

Makala iliyopita
Makala ijayo

2 Komentara

    Habari hii iko vyema.

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe