Mabingwa hao mara 20 wa Uingereza hawatarajii kunua wachezaji wapya mwezi Januari, lakini kuna uwezekano wa kuwauza wachezaji kadhaa pale Old Trafford wakati United wakijaribu kupunguza kikosi chao.
Kwa mujibu wa Manchester Evening News, takribani wachezaji watano wa kikosi cha kwanza wanaweza kuondoka, akiwemo Anthony Martial, ambaye ameonyesha nia ya kutafuta klabu mpya mwanzoni mwa 2022.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo pia inadai kuwa Jesse Lingard, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao wa joto na mlinda mlango nambari mbili Dean Henderson wanaweza kuondoka katika dirisha la Januari, huku mustakabali wa Donny van de Beek unaendelea kutiliwa shaka.
Man United pia inadaiwa kufikiria kumuuza Paul Pogba kwa pesa zinazofaa mwezi ujao, huku mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa katika klabu hiyo ukikamilika Juni ujao.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

