West Ham Kila kitu Sawa kwa Todibo

Klabu ya West Ham iko mbioni kukamilisha dili la beki wa klabu ya OGC Nice raia wa kimataifa wa Ufaransa Jean Clair Todibo ambaye wamekua wakimfuatilia kwa wiki kadhaa.

West Ham wamekubaliana na klabu ya OGC Nice kumsajili beki huyo kwa kiasi cha kwa mkopo wa msimu mzima ambao hauna kipengele cha kumnunua, Hii imekuja baada ya klabu ya Juventus kushindwa kulipa kiasi ambacho kilikua kinahitajika kwa beki huyo.west hamMsimu huu wagonga nyundo hao kutoka jiji la London wameonekana kua makini katika sajili ikiwa ni baada ya kutofanya vizuri msimu ulimalzika chini ya kocha David Moyes ambaye wameachana nae, Kocha Julein Lopetegui ameonekana kufanya mabadiliko makubwa ndani ya timu hiyo kwa kipindi cha muda mfupi.

Beki Todibo inaelezwa alikubaliana maslahi binafsi na klabu ya Juventus lakini kilichoshindikana kwa vibibi vizee hao wa Turin ni kulipa kiwango ambacho klabu ya OGC Nice walikihitaji, Hivo klabu hiyo ya West Ham wakatumia fursa ya Juventus kufeli kulipa ada ya uhamisho ambapo wao wameweza kutumia ushawishi wao kumpata Todibo.

Acha ujumbe