Westham Kumchukua Kyle Walker

Klabu ya Westham ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Southampton kwajili ya kumsajili beki wa kulia wa klabu hiyo Kyle Walker Peters kwa kubadilishana na mchezaji mwingine katika dirisha hili kubwa.

Westham wako tayari kumuachia mchezaji wake Flynn Downes kwajili ya kumpata beki Kyle Walker Peters ambaye amekua akionesha kiwnago bora sana kwa takribani misimu mitatu sasa ndani ya klabu ya Southampton ambayo imerejea ligi kuu msimu huu.westhamVilabu hivo vinaelezwa kufikia hatua nzuri kwajili ya kufanya dili hilo la kubadilishana wachezaji ambapo kila klabu imeridhia kupata hudumu ya mchezaji kutoka timu nyingine, Hii msimu huu inatokea kwa mara ya pili kwani tayari klabu ya Aston Villa imefanya biashara ya namna hii na klabu ya Juventus.

Beki wa kulia wa Southampton inaelezwa yeye tayari ameshakubali kujiunga na wagonga nyundo kutoka jiji la London klabu ya Westham, Hivo kinachosubiriwa mpaka sasa ni kukamilika kwa mazungumzo ya mwisho yanayovihusu vilabu hivo ili kila klabu impate mchezaji wake.

Acha ujumbe