Mchezaji wa Westham United Jarrod Bowen msimu uliopita alikuwa na kiwango kikubwa msimu uliopita, lakini anajitahidi kufikia matarajio yaleyale wakati huu. Baada ya kutoka nyuma kabisa mchezaji huyo wa Westham alitabiriwa kuendelea katika mkondo huo huo na kushinikiza nafasi katika kikosi cha Gareth Southgate Kombe la Dunia.

 

Westham Yamtaka Bowen Arudi kwenye Ubora Wake.

 

Hata hivyo, ingawa uchezaji wake barani Ulaya umekuwa wa kutia moyo, kiwango cha mshambuliaji  kwenye ligi kuu kimeshindwa kufikia viwango vyake vya juu.  Bowen hadi sasa bado ana matarajio ya kuitwa kwenye kikosi cha England kitakachoshiriki kombe la Dunia 2022 huko Qatar.

Msimu uliopita ulikuwa wenye tija zaidi katika maisha ya Bowen ya ligi kuu hadi sasa. Alikuwa kiungo muhimu sana kwa Westham kwani waliweza kumaliza katika nafasi ya saba ya ligi kuu ya Uingereza na kufika nusu fainali ya Europa ambapo Westham mbele ya Frankfurt ambao ndio walitwaa taji hilo.

 

Westham Yamtaka Bowen Arudi kwenye Ubora Wake.

Mchango wake katika eneo la ushambuliaji ulikuwa wa muhimu huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akifunga mabao 18 na kutoa pasi za mabao 11 katika mashindano yote . Kutokana na kiwango hicho, Bowen alimvutia kocha wa Southgate na kumpa nafasi ya kucheza mechi nne za kwanza za Kimataifa mwezi Juni.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa