Wijnaldum: Unabaki au Unaondoka Anfield??

Tunaendelea tulipoishia kwenye sakata la Georginio Wijnaldum ndani ya kikosi cha Liverpool. Swali ni kwamba, tunabaki au tunaondoka Anfield?

Gini Wijnaldum kama ambavyo kocha wake (Jurgen Klopp) anapenda kumuita, anaingia kwenye miezi 6 ya mwisho kwenye mkataba wake na Liverpool.

Licha ya mabosi wa klabu hiyo kumpatia kandarasi mpya ili aendelee kubaki Anfield, Wijnaldum amewasubirisha viongozi wa klabu hiyo wakati huu ambao bado anafikiria ni uamuzi upi sahihi kwake kuufanya – abaki au aondoke?

Upande wa pili wa vuguvugu hili kuna Ronald Koeman ambaye ni dhahiri anamuhitaji Gini kwenye kikosi chake kule Catalunya akiwa na Barcelona.

Georginio akiwa na Koeman kwenye Timu ya Taifa ya Uholanzi.

Majira ya kiangazi, Koeman aliweka wazi matamanio yake ya kumsajili kiungo huyu ambaye alifanya nae kazi kubwa na nzuri wakati walipokuwa pamoja kwenye timu ya taifa ya Uholanzi.

Wiki ya kufanya maamuzi ni hii. Dirisha dogo la usajili litafunguliwa rasmi Januari 2,2021 na Gini atakuwa na jukumu la kuamua hatma yake. Ni asaini mkataba wa mapema na Barcelona ili ajiunge nayo msimu ujao au aongeze mkataba Anfield.

Hapa ni vita ya Klopp vs Koeman, nani atafanikiwa kumpata Wijnaldum kwenye kikosi chake kuanzia msimu ujao?

Wiki hii pengine majibu sahihi yatapatikana, waswahili walisema ‘kizuri chajiuza’.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

21 Komentara

    Ni maamuzi sahihi

    Jibu

    Nimaamuzi yake mwenyewe

    Jibu

    Safi ayo ni mamuzi yke mwenyewe

    Jibu

    Maamuzi ni yake

    Jibu

    Mwenye kisu kikali atakula nyama

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Maamuzi mazuri

    Jibu

    Dogo abaki tu liverpool mbona ni klabu bora

    Jibu

    Kila mtu na maamuzi yake

    Jibu

    Upande wa pili wa vuguvugu hili kuna Ronald Koeman ambaye ni dhahiri anamuhitaji Gini kwenye kikosi chake kule Catalunya akiwa na Barcelona.

    Jibu

    Maamuzi ni yake

    Jibu

    Ngoja tuone nimamuzi yake abaki au asepe

    Jibu

    Maamuz ni yake

    Jibu

    Hiyo ataamua mwenyewe

    Jibu

    Yuko sahihi kabisaa

    Jibu

    Kazi kwake kuchagua

    Jibu

    Lazima ataondoka tuu

    Jibu

    Aende tu kwani yeye si kama Messi wa kukaa kila siku barca

    Jibu

    Maamuzi ni yake

    Jibu

Acha ujumbe