Klabu ya Wolves inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imefanikiwa kumrudisha beki wake wa kulia ambaye alikua klabu ya Tottenham Hotspurs na baadae kutimkia Atletico Madrid Matt Doherty.
Matt Doherty alijiunga na klabu ya Tottenham kabla ya kwenda misimu miwili nyuma akitokea klabu ya Wolves na lakini mbwa mwitu hao wameamua kumrudisha beki huyo akitokea klabu hiyo kutoka kaskazini mwa jiji la London.Beki Matty Doherty amekua hapati nafasi mara kwa mara ndani ya kikosi cha Tottenham kutokana kupata majeraha ya mara kwa mara ikiwa ndio sababu ya yeye kutokupata nafasi kwenye kikosi cha Spurs na baadae kuelekea Atletico Madrid ya nchini Hispania.
Wolves wamemrudisha beki huyo wa kimataifa wa jamhuri ya Ireland kwajili ya kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao ambapo beki huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu mkataba ambao utamueka klabuni hapo mpaka mwaka 2026.