Mwamuzi wa Somalia Anyimwa Kuingia Marekani kwa Ajili ya Kombe la Dunia.

Mwamuzi kutoka Somalia ambaye alikuwa amepangwa kuchezesha mechi za Kombe la Dunia 2026 amenyimwa ruhusa ya kuingia nchini Marekani.

Mwamuzi wa Somalia Anyimwa Kuingia Marekani kwa Ajili ya Kombe la Dunia.

Omar Artan, ambaye alikuwa anatarajiwa kuwa Msomali wa kwanza kuwahi kuchezesha mechi ya Kombe la Dunia, alizuiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami baada ya kuwasili kutoka Istanbul siku ya Jumamosi.

Baada ya kufanyiwa ukaguzi, alinyimwa kuingia nchini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni “wasiwasi wa kiusalama katika mchakato wa uhakiki wa taarifa zake” (vetting concerns), kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani (CBP).

CBP haikutaja jina la Artan moja kwa moja katika taarifa yake, lakini ndiye mwamuzi pekee kutoka Somalia aliyekuwa ameteuliwa kushiriki Kombe la Dunia.

FIFA ilithibitisha Jumatatu kuwa Artan hataweza kushiriki mazoezi wala kuchezesha mechi katika mashindano hayo yatakayoanza tarehe 11 Juni nchini Marekani, Mexico na Canada, huku mechi nyingi zikichezwa nchini Marekani.

“Licha ya hali hii, bado nina ari nzuri na nimeelekeza mawazo yangu kwenye changamoto zinazofuata katika kazi yangu ya uamuzi,” alisema Artan katika taarifa yake. Mwamuzi huyo alitunukiwa tuzo ya Mwamuzi Bora wa Mwaka ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwaka 2025.

Mwamuzi wa Somalia Anyimwa Kuingia Marekani kwa Ajili ya Kombe la Dunia.

“Ningependa kuishukuru FIFA na Shirikisho la Soka Afrika kwa msaada wao wote, na ninaahidi kuendelea kuboresha kiwango changu cha uamuzi huku nikielekeza nguvu zangu kwenye siku zijazo.

“Ninashukuru familia ya soka kwa ujumbe wao wa kunitia moyo, na ninawatakia wenzangu mafanikio makubwa katika Kombe la Dunia. Natarajia kuungana nao tena katika mashindano yajayo.”

Katika taarifa yake, FIFA ilisema kuwa haijihusishi na taratibu za uhamiaji na kwamba iliarifiwa na mamlaka husika kuwa hali ya Omar Artan “haitabadilishwa kwa sasa.”

“Kwa kuzingatia utaratibu uliotumika katika mashindano ya FIFA yaliyopita, serikali ya nchi mwenyeji ndiyo yenye mamlaka ya mwisho kuamua nani atapewa visa na nani ataruhusiwa kuingia nchini. Rais wa Marekani, Donald Trump, alisitisha kuingia kwa raia wa Somalia kupitia tangazo la mwezi Juni 2025, akiitaja Somalia kuwa “mahali salama kwa magaidi.” Ilisema FIFA.

Hatua hiyo ilifuatia amri ya kiutendaji ya Januari 2025 iliyotaka serikali kutoa ripoti kuhusu nchi ambazo zilionekana kuwa na mapungufu katika mifumo ya uhakiki na uchunguzi wa taarifa za wasafiri, kama sehemu ya kampeni ya kuimarisha udhibiti wa uhamiaji.

Pia, kuingia kwa raia kutoka Afghanistan, Myanmar (Burma), Chad, Jamhuri ya Congo, Equatorial Guinea, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Sudan na Yemen kumesitishwa.

Mwamuzi wa Somalia Anyimwa Kuingia Marekani kwa Ajili ya Kombe la Dunia.

Katika taarifa yake, Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani (CBP) ilisema kuwa wasafiri wote wanaoingia nchini humo hupitia mchakato wa ukaguzi na uhakiki.

“Wakati wa uchakataji wa taarifa zake, msafiri huyo alipitia ukaguzi wa ziada, ambao ni sehemu ya kawaida ya utaratibu wa CBP pale maafisa wanapohitaji kuthibitisha taarifa au kuamua kama mtu anaruhusiwa kuingia nchini,” ilisema taarifa hiyo.

“Baada ya ukaguzi, msafiri huyo, ambaye ni mwamuzi wa Kombe la Dunia la FIFA, alibainika kutokidhi masharti ya kuingia nchini kutokana na masuala yaliyobainika katika mchakato wa uhakiki wa taarifa zake, hivyo akanyimwa kuingia.”

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa maamuzi kuhusu kuruhusiwa kuingia nchini hufanywa kwa kuzingatia kila kesi kivyake, kwa kutumia taarifa za vyombo vya sheria, usalama wa taifa na uhamiaji zinazopatikana wakati wa ukaguzi.

“Maafisa wa CBP wana mamlaka ya kuwahoji wasafiri, kufanya ukaguzi na kuamua iwapo wanaruhusiwa kuingia nchini kwa mujibu wa sheria za Marekani.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.