Nahodha wa timu ya taifa ya Marekani, Tim Ream, amewataka wachezaji wenzake kuikumbatia presha ya kucheza Kombe la Dunia 2026 nyumbani, akieleza kuwa ni nafasi ya kipekee ambayo inaweza kutokea mara moja tu katika maisha ya mchezaji wa soka.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Hii ni fursa ya mara moja katika maisha ya mchezaji. Kuna matarajio makubwa na presha zaidi, lakini hakuna anayetuongezea presha kuliko sisi wenyewe. Tunapaswa kuifurahia nafasi hii maalum,” alisema Ream wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Beki huyo mwenye uzoefu alifichua kuwa amekuwa akiwahamasisha wachezaji vijana wa kikosi hicho kufungua macho yao na kufurahia kila hatua ya mashindano hayo, akisisitiza kuwa kucheza Kombe la Dunia nyumbani ni jambo la kipekee ambalo huenda lisijirudie tena katika maisha yao ya soka.
Mshambuliaji Folarin Balogun alisema kushiriki Kombe la Dunia akiwa na Marekani mbele ya mashabiki wa nyumbani ni jambo lenye hisia kubwa kwake kutokana na safari yake ya maisha. “Kuwakilisha taifa langu mbele ya mashabiki wa nyumbani ni jambo maalum sana kwangu, kwa familia yangu, marafiki zangu na timu yetu,” alisema nyota huyo aliyezaliwa Marekani na kukulia England.
Kwa upande wake, mshambuliaji Ricardo Pepi na kipa Matt Freese walisema kikosi hicho kinaamini Kombe la Dunia ni fursa ya kuonyesha uwezo wao mbele ya dunia. “Tunaliangalia kama jambo la kipekee la kuiwakilisha nchi yetu mbele ya watu wetu,” alisema Pepi, huku Freese akiongeza, “Unaota kupata nafasi kama hii kwa miaka mingi. Presha hutengeneza almasi, na tunaamini sisi ni kundi la wachezaji 26 walio tayari kuthibitisha hilo katika Kombe la Dunia.”


