Uingereza Yapata Hofu Kuhusu Ugonjwa wa Declan Rice Kuelekea Mechi ya Norway

Uingereza inakabiliwa na kipindi cha kusubiri kwa wasiwasi kabla ya mchezo wake wa robo fainali ya Taji la Dunia dhidi ya Norway baada ya ugonjwa kuikumba kambi yao iliyopo Miami.

Uingereza Yapata Hofu Kuhusu Ugonjwa wa Declan Rice Kuelekea Mechi ya Norway

Kiungo Declan Rice amekosa mazoezi mawili mfululizo, hali ambayo imemfanya kocha Thomas Tuchel kuwa na hofu kubwa kuhusu uwepo wake katika mchezo huo, huku benchi la ufundi likifanya kila liwezalo kuzuia ugonjwa huo usisambae kwa wachezaji wengine ndani ya kikosi.

Hali ya ndani katika kambi ya timu ya taifa ya Uingereza imegubikwa na wasiwasi mkubwa baada ya Declan Rice kukosa mazoezi ya pili mfululizo kuelekea mchezo wa robo fainali ya Taji la Dunia dhidi ya Norway siku ya Jumamosi.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 anaripotiwa kuugua ugonjwa wa tumbo (sickness bug), huku BBC ikieleza kuwa hali yake imezidi kuwa ngumu kutokana na ugonjwa huo pamoja na tatizo lililokuwepo awali la mishipa ya fahamu katika eneo la misuli ya nyuma ya paja (hamstring) na mgongo wa chini.

Wahudumu wa afya wa Three Lions sasa wanafanya haraka kudhibiti hali hiyo na kumtenga anayehusika ili kuzuia ugonjwa huo usisambae kwa wachezaji wengi ndani ya kikosi.

Uingereza Yapata Hofu Kuhusu Ugonjwa wa Declan Rice Kuelekea Mechi ya Norway

Wakati huohuo, kocha Thomas Tuchel wa Uingereza anatakiwa pia kufuatilia hali ya beki Marc Guéhi, ambaye anaendelea kuuguza majeraha ya misuli ya nyuma ya paja (hamstring).

Ripoti za mlipuko wa virusi hazijaikumba tu kambi ya Uingereza, bali pia ziliripotiwa kwa muda mfupi katika kituo cha mazoezi cha Norway nchini Marekani.

Nahodha wa Norway, Martin Ødegaard, awali alithibitisha kuwa baadhi ya wachezaji na viongozi wa timu hiyo walikuwa wakijisikia vibaya kutokana na mabadiliko makubwa ya hali ya joto.

Kiungo huyo wa Arsenal alisema: “Ndiyo, imekuwa hivyo kidogo. Nadhani unapobadilisha hali ya joto, matumizi ya kiyoyozi na mambo mengine kama hayo, ni jambo la kawaida. Kwa kweli si tatizo kubwa. Lakini tumekuwa na baadhi ya watu wakijisikia vibaya kidogo, ingawa si jambo kubwa na tunapaswa kuwa tayari kabisa kwa Jumamosi.”

Licha ya nahodha wake kukiri kuwa kulikuwa na changamoto ndogo za kiafya ndani ya kikosi, kocha wa Norway, Ståle Solbakken, alichukua hatua haraka kupunguza hofu iliyokuwa ikienezwa na vyombo vya habari.

Uingereza Yapata Hofu Kuhusu Ugonjwa wa Declan Rice Kuelekea Mechi ya Norway

Solbakken alisisitiza kuwa taarifa za ugonjwa unaosambaa miongoni mwa wachezaji wake ni uvumi tu, akieleza kuwa kila mmoja katika kikosi chake yuko katika hali nzuri kiafya na yuko tayari kwa mchezo.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 alisema: “Nadhani suala la ugonjwa ni uvumi. Ødegaard ambaye anaumwa ni mjomba wake Martin ambaye ni mtaalamu wa tiba ya viungo (physio), si Martin mwenyewe. Kwa hiyo kila kitu kiko sawa, kila mchezaji yuko vizuri, hakuna ugonjwa wowote miongoni mwa wachezaji. Kuna mmoja au wawili waliowahi kuwa na tatizo hilo kwenye benchi la ufundi. Kwa sasa, sote tuko tayari kuingia uwanjani.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.