Xavi Aanza kwa Kutumbua Majipu Barca

Mapema tuu baada ya Xavi kuchukua rasmi kibarua cha umeneja klabuni Barcelona, ameamua kuanza kupangua na kupanga sehemu ambazo zinahitaji mabadiliko.

Nyota huyu wa zamani wa Barcelona, alikamilisha taratibu za kuwa menaja kwa Barcelona wikiendi, na kutangazwa rasmi kwa mashabiki kama Meneja mpya Camp Nou Jumatatu.

Xavi anaungana na Barcelona ambayo inapitia kipindi kigumu cha changamoto ya uchumi na changamoto ya majeraha.

Kwa sasa, Xavi ameamua kuanza na changamoto ya majeraha, ambalo ni suala lililo ndani ya uwezo wake.

Xavi Aanza kwa Kutumbua Majipu Barca

Kwa mujibu wa Diario As, Xavi hawahitaji tena mtaalamu wa mazoezi ya mwili Juanjo Brau na mkufunzi wa mazoezi viungo Albert Roca.

Taarifa zinasema kuwa Jaume Munill anaweza kurejea klabuni hapo baada ya kuondoka miaka miwili iliyopita, akiungana na Ricard Pruna ambaye pia amewahi kufanya kazi Barcelona miaka ya nyuma.

Kutokana na changamoto ya majeraha, meneja huyu anaamini hiyo ni hatua ya kwanza kuelekea kupata suluhisho.


NJIA RAHISI YA MKWANJA NA TITAN DICE

Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe