Hazard Awachana Madrid Kutaka Kusepa!

Eden Hazard anaweza akaondoka klabuni Real Madrid kabla ya wakati wa mkataba wake kuisha.

Miaka miwili iliyopita imekuwa ni kipindi kigumu sana kwa staa huyu wa Ubelgiji ambaye amekuwa akipambania kurejea kwenye fomu pamoja na hali yake ya fanya akikutana na misuko suko kadhaa ya majeraha.

Licha ya majeraha kumkwamisha zaidi Eden Hazard, suala la kupata nafasi kwenye kikosi pia limekuwa changamoto pale anapokuwa mzima wa afya.

Eden Hazard
Eden Hazard

Mastaa kama Rodrygo na Vinicius Junior wamemkimbiza Hazard msimu huu, huku staa huyu akikosa kuchaguliwa kwenye kikosi cha gemu muhimu.

Taarifa zinasema kuwa staa huyu amesema sasa basi, anataka kwenda kupambana na changamoto zingine mahali pengine. Je Real watamruhusu?

Taarifa zinasema kuwa anaweza kuingia sokoni. Taarifa zaidi za chini ya kapeti zinasema staa huyua anaonekana kuwa na changamoto ingine ya kiafanya ambayo anahitaji kufanyiwa upasuaji, na Florentino Perez anatajwa kuwa ameshauri aepuke upasuaji ili aweze kuuzika sokoni.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe