Kocha wa Barcelona Xavi ameripotiwa kukubali kwamba klabu hiyo ya Catalan haitaweza kumsajili Ousmane Dembele kwa kumuongezea mkataba mpya. Taarifa zinataja kuwa staa huyu anaenda Juventus au Man United
Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 huko Camp Nou unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, kwa sasa yuko huru kujadili mkataba wa awali na klabu za kigeni.
Xavi hapo awali amekuwa na matumaini linapokuja suala la uwezekano wa Barcelona kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa kumungezea mkataba klabuni hapo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa AS, kocha mkuu wa klabu hiyo ya Catalan sasa amekosa subira na hali hiyo na amekubali kuwa makubaliano juu ya mkataba mpya yamegonga mwamba.

Ripoti hiyo inadai kuwa Barcelona wamekasirishwa na mahitaji ya wakala wa Dembele Moussa Sissoko huku kukiwa na mapendekezo kwamba Mfaransa huyo anataka mkataba wenye thamani ya £700,000 kwa wiki.
Hata hivyo, Sissoko hivi majuzi alisisitiza kuwa kukwama kwa mazungumzo ya mkataba hakukutokana na masuala ya fedha.
Juventus na Manchester United wanadaiwa kushindania nafasi ya kumsaini ya Mfaransa huyo kwa uhamisho wa bure kabla ya kampeni za 2022-23.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

CHEZA HAPA

