Kocha mkuu wa Barcelona Xavi Hernandez anaamini kuwa Sheikh Jassim bin Hamad bin Al Thani ndiye anayefaa kuwa mmiliki wa Manchester United.
Al Thani aliongoza moja ya zabuni mbili za umma kwa United kabla ya tarehe ya mwisho kuimiliki timu hiyo wiki iliyopita. Kiasi kidogo inajulikana kuhusu benki ya Qatar, ambaye anatarajia kununua asilimia 100 ya klabu baada ya familia ya Glazer kuweka hisa zao kwa mauzo.
Lakini Xavi, ambaye anakabiliana leo na United kwenye mchezo wa Europa mkondo wa pili, alitumia miaka miwili na nusu kuifundisha Al Sadd ya Qatar.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 43 pia awali alikuwa mchezaji wa Al Sadd na anamfahamu Al Thani hivyo amesema kuwa ni mtu anayewajibika, mwenye umakini, anayefaa kwa United kwani alifanya kazi Qatar kwa miaka sita na anamfahamu Sheikh.