Mchezaji wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Spain Xavi Hernandez, amethibitisha kupona maradhi yaliyokuwa yana mkabili na amerudi katika shughuli yake ya kuifundisha timu ya Al Sadd.

Xavi mwenye umri wa miaka 40 alithibitika kupata maambukizi ya Virusi vya Corona na alijitenga kwa muda ili asisambaze kwa wengine.

Hii inamaanisha alikosa mchezo dhidi ya Al Khor na nafasi yake ilichukuliwa na kocha msaidizi na Al Sadd walishinda mchezo huo 2-1 kwenye michuano ya Qatar Stars League, lakini Xavi yupo vizuri tena alisema kupitia Instagram.

Kiungo huyo wa zamani amekuwa akihusishwa na kuhamia kunako ligi ya LaLiga katika timu yake ya zamani ya Barcelona, aliweka picha yake mwenyewe akiwa nyumbani na watoto wake.

Katika chapisho alililoweka siku ya Jumatano, Xavi aliwashukuru watu wanaomfuatilia katika akaunti yake ya Instagram kwa kumjulia hali na kumuonesha kujali tangu atangaze amepata maambukizi ya COVID-19.

“Nataka kujumuika nanyi kwamba nimepona na narudi nyumbani kuiona familia yangu na kisha nitaungana na timu yangu @alsaddsc”.

Katika posti tofauti tofauti Al Sadd pia walionesha Xavi akiwa katika mjukumu yake katika klabu akiwa amevaa barakoa na kumkaribisha mchezaji mpya aliye sajiliwa Rodrigo Tabata.


Nini kinachokupa raha kama michezo ya kasino ya mtandaoni? Hasa unapojua kuwa kuna ushindi, jackpot na mizunguko kibao ya bure.
Ungana na bwana Meridian kupata ushindi na burudani.

Cheza hapa sasa

45 MAONI

  1. Habari nzuri sana kwa timu ya Al Sadd kuendelea kunolewa na kocha wao mkuu, Tunamuombea Xavi afya njema zaidi na zaidi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa