Xavi Awakataa Mane na Aubameyang Barcelona!

Nyota wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Xavi Iniesta amepinga vikali mpango wa klabu yake ya zamani ‘Barcelona’ kuwasajili wachezaji Pierre-Emerick Aubameyang na Sadio Mane.

Pierre-Emerick Aubameyang wa Arsenal na Sadio Mane wa Liverpool kama walikuwa na ndoto za kuchezea Barcelona katika maisha yao ya soka basi walifikirie vizuri wazo lao hilo.

Xavi Hernandez ambaye ni zao la shule ya michezo ya Barcelona ‘La masia’ anaamini kuwa Mane na Aunameyang hatoweza kumudu mtindo wa uchezaji soka wa Barcelona.

Xavi hana shida na uwezo wa wachezaji hao, lakini wasiwasi wake ni juu ya aina ya uchezaji wa wachezaji hao kumudu kuingia katika mfumo wa klabu ya Barcelona.

Mkataba wa Aubameyang na Arsenal unaelekea mwishoni kabisa na Aunameyang amegoma kabisa kusaini mkataba mpya na vigogo hao wa London pamoja na kuweka wazi ndoto zake za kuchezea ligi ya Hispania maarufu kama La Liga.

Kwa upande wa Sadio Mane yeye bado ana mkataba mrefu na Liverpool mpaka mwaka 2023 lakini kwa muda mrefu amekua akihusishwa na kuhitajika na kikosi cha Barcelona.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2018/19 ulikua msimu wa mafanikio makubwa kwa wote hawa wawili baada ya kumaliza wote kuibuka vinara wa ufungaji katika ligi kuu ya EPL. Wawili hao walishinda tuzo ya kiatu cha dhahabu pamoja na nyota mwingine wa mafarao wa Misri, Muhammed Sallah.

Wakati dunia inawatazama Aunameyang na Mane kama wachezaji hatari nanwenye uwezo wa hali ya juu wa kufunga, yeye Xavi anawatazama kama wenye uwezo wa kawaida tu na wanaweza kufunga pale tu ambapo kuna nafasi za wazi huku Barcelona ikihitaji wachezaji wawezao kutembea katika nafasi finyu na kuleta madhara kwa mpinzani.

Maoni haya ya Xavi yanaweza kupingwa na wadau wengi wa soka kwa sababu mbalimbali. Binafsi ninamuunga mkono kwa sababu kuu mbili;

Kwanza, Xavi anaijua vema Barcelona. Anajua ni nini inahitaji kwa wakati gani na nini haihitaji. Ikumbukee kuwa Xavi ni zao la shule ya vipajo ya Barcelona, La Masia na alijiunga hapo tangu akiwa na miaka 11! Amekua na Barcelona katika hali zote, amevuja jasho na damu kuiongoza Barcelona kushinda taji la La liga mara nane huku wakishinda ligi kuu ya mabingwa Ulaya ‘UEFA’ mara nne! Hivyo basi ni wazi kuwa Xavi anaijua vema falsafa ya soka la Barcelona ya ‘tik-tak’. Mfumo wa pasi fupifupi zikipigwa katika njia sahihi na timu ikicheza kama timu zaidi badala ya mchezaji mmoja mmoja kucheza katika nafasi yake tu.

Pili, Xavi hivi sasa ni kocha wa timu ya Al Sadd inayoshiriki ligi kuu ya Qatar.kwa hiyo ni wazi kuwa hatoi maoni ya kishabiki bali ya kitaalamu kama mwalimu wa soka.

Sababu hizo mbili zinatosha kabisa kumfanya mtu hata kama hakubaliani moja kwa moja na maoni ya Xavi basi angalau ayafikirie kwa mara ya pili.

25 Komentara

    Ni maoni yake, sio kiongozi wa timu na uongozi wa sasa unaweza kuamua kinyume chake#Meridianbettz

    Jibu

    Xavi yuko sahihi

    Jibu

    Kwa maoni yake yeye kaona hawafai

    Jibu

    Uongozi uyafanyie kazi maoni yake

    Jibu

    ayo n maoni yake

    Jibu

    xavi kazeeka umri hadi akili, maana sio kwa kuwakataa hawa jamaa, hata kama mfumo ni mgeni kwao, ndio maana akawepo kocha kwa ajili hiyooo!!

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Huo ni mtazamo wake

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Ayo ni maono yake ila wako vizuri uongozi ukiwaitaji uwachukue tu wako vizuri sana

    Jibu

    Yupo sahh kwa utamaduni wa wakatalunya thnks meridian bet kwa information

    Jibu

    Xavi yupo vizuri..!uwongozi uwangalie maamuzi yake

    Jibu

    Huo ni mtazamo wako

    Jibu

    Makala nimeipenda ngoja tusubili maamuzi ya management ya Barcelona

    Jibu

    Xavi atakuwa na chembechembe za ubaguzi

    Jibu

    Maoni yake nazuri

    Jibu

    uongozi ufanyie kazi maoni yake

    Jibu

    Xavi yuko sahihi

    Jibu

    sisi mashabiki tunaona wako vizuri

    Jibu

    Mtazomo wake! Mane ni Bora kwa sasa
    Fundi wa mpira.#meridianbettz

    Jibu

    Mtazamo wake!mane ni Bora kwa sasa fundi wa mpira# meridianbettz

    Jibu

    Ikumbukwe Lamasia siku hizi imekuwa haina vipaji vy akutisha lakini ukiwaangalia hawa jamaa ni wachezaji ambao wamekuwa wakisumbua ulimwengu wa soka kwa sasa!!! Hapa Xavi kapuyanga

    Jibu

    sasa mane na pierre inabidi wakathibitishe kuwa xavi kakosea kuwa kana

    Jibu

    Ni kweli hawaendani na aina ya mpira unaopigwa barca …NAUNGANA NA KAULI YA FUNDI XAVI

    Jibu

    Good news

    Jibu

Acha ujumbe