Kocha wa klabu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez amezungumza kua hawatakata tamaa licha ya ugumu uliopo mbele kwenye kufuzu hatua ya ya 16 kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya.
Klabu ya Barcrlona inakabiliwa na wakati mgumu sana katika michuano ya ulaya kwani wanahitajika kushinda michezo miwili iliyobakia katika ligi ya Mabingwa huku wakiomba klabu ya Inter Milan ipoteze mchezo mmoja kati ya miwili iliyobakiza.
Fc Barcelona kesho itashuka dimbani katika uwanja wake wa nyumbani wa Camp Nou kuwakaribisha klabu ya Fc Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa tano wa ligi ya mabingwa ulaya huku Barcelona wakihitajika kushinda mchezo ili kuendelea kuweka matumaini ya kupata nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.Kocha Xavi amesema vijana wake wanatakiwa kupambana bila kujali matokeo yatakuaje katika mchezo wa klabu a Inter Milan ambao watacheza na timu inayoshika mkia cha msingi ni kupambana kuelekea mchezo huo.
Xavi bado amesisitiza kudondokea kwenye michuano ya Europa kama timu hawajafikiria na kua hawajakata tamaa na watapigana kama Simba kuhakikisha wanabaki na kukata tamaa hakuna nafasi.