Xavi Hernandezkocha wa klabu ya Barcelona ameonesha kukasirishwa na matokeo yalityotokea katika mchezo wa jana dhidi ya klabu ya Interzionale Milan ambapo walifungwa bao moja kwa bila na kudai hawakutendewa haki katika mchezo huo.

xavi hernandezKatika mchezo huo ambapo Hakan Calhanoglu aliiweka Inter Milan mbele kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika na klabu ya Barcelona wakiamini wangeweza kurudi mchezoni baada ya kua waliutawala mchezo huo.

Hali haikua hivo kwani Inter Milan walifanikiwa kucheza vizuri na ka nidhamu ya hali ya juu na kulinda bao hilo na kufanikiwa kumaliza mchezo huo wakishinda bao moja kwa bila dhidi ya Barcelona.

Xavi Hernandez aliamini kama wameonewa katika mchezo kutokana na tukio lililotokea baada ya baada ya bao lao lililofungwa na kinda wa kihispaniaola Pedri kukataliwa baada ya marudio ya VAR na kuonesha mpira wa krosi uliopigwa na Dembele uliokolea na kipa Andre Onana na kutua kwenye mkono wa Ansu Fati hivo kufanya lisiwe bao.

xavi hernandezXavi Hernandez aliondoka kwenye mchezo huo huku akitupa lawama kwa waamuzi wa mchezo huo na kuweka wazi kukasirishwa na kitendo kilichotokea kwenye mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa