Xavi: Milango Iko Wazi kwa Messi

Kocha wa klabu Barcelona Xavi Hernandez siku ya jumamosi wakati akiwa kwenye kikao na waandishi wa habari alisema kuwa milango iko wazi kwa aliyekuwa nyota wa timu hiyo Lionel Messi kurejea kwenye viunga vya Camp Nuo.

Messi ambaye aliondola kwenye klabu hiyo kwa uhamisho huru, baada ya kushindikana kusaini mkataba mpya kutokana na matatizo ya kifedha ambayo klabu ya Barcelona inapitia.

Xavi
Xavi Hernandez akiwa kwenye kikao na waandishi kabla ya mchezo wa El Clasico

Xavi alipoulizwa ikiwa milango iko wazi kwa mshambuliaji huyo kurejea alijibu, “Messi ni mchezaji bora wa kihistoria na kwenye historia ya klabu, ana haki ya kurejea na milango iko wazi kwake.

“Ilimradi mimi ni kocha hapa milango iko wazi kwake ikiwa atahitaji kurejea siku yoyote. Messi ni mchezji bora wa kihistoria na kama klabu tunampa heshima kubwa, anayostahili, lakini ana mkataba na PSG, kuna machache naweza kukuambia.

“Ikiwa atahitaji kuja siku yoyote, kuangalia mazoezi, kuzungumza na wakufunzi, milango iko wazi kwa sababu ni mchezaji bora wa kihistoria kwenye klabu hii.”

Tokea Messi aondoke klabu ya Barcelona haikuwa na muendelezo mzuri, mpaka alipochaguliwa Xavi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, ndio alieleta matumaini mapya kwenye klabu hiyo.

Barcelona leo wanajiandaa kukutana na Real Madrid kwenye El Clasico, huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza michezo mitano mfulululizo kwenye El Clasico. Je xavi atapindua meza leo.

SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe