Kiungo wa kati wa klabu ya Arsenal, Granit Xhaka anatarajiwa kuwa nje kwa miezi mitatu baada ya kuumia goti katika dabi ya London walioibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Tottenham.

 


Xhaka aligongwa kwa bahati mbaya na Lucas Moura baada ya mchezaji huyo kuchezewa madhambi na Thomas Partey na kudondoka chini katika harakati za Tottenham kujitafutia goli la kufuta machozi.

Mchezaji huyo alitolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Albert Sambi Lokonga na taarifa zilizothibitishwa mchezaji huyo ataukosa mwaka wote wa 2021.

“Kulingana na uchunguzi zaidi uliofanywa katika jeraha la goti la kulia katika ya mechi dhidi ya Tottenham, Uchunguzi na vipimo vinadhibitisha Granit Xhaka amepata jeraha baya katika goti lake.” ilisomeka taarifa ya Arsenal.

“Wataalamu walifanya kikao London, siku ya Jumanne jioni na kugundua Granit haitaji upasuaji.

” Programu ya kurejea na kupona itaanza mara moja na tunatarajia atarejea baada ya miezi mitatu.

“Kila mtu ndani ya klabu anamsapoti na kufanya kazi kwa bidii na Granit kuweza kumrejesha uwanjani haraka iwezekanavyo.” ilimaliza taarifa hiyo.


SPACE SPIN NA MERIDIANBET.

Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa