Xhavi: "Lewandowski Ndiye Mfungaji Bora Duniani".

Kocha mkuu wa Barcelona Xhavi Hernandez amesema kuwa mshambuliaji wake Roberto Lewandowski ni mchezaji ambaye anakupa dhamana na hilo liko wazi sana.

 

Xhavi: "Lewandowski Ndiye Mfungaji Bora Duniani".

Xhavi ameyasema hayo hapo jana baada ya Lewandowski  kuipatia timu yake alama tatu muhimu kwa kufunga bao 1-0 dhidi ya Mallorca  kwenye Laliga, na mchezo kumalizika kwa Barca kushinda bao hilo hilo moja.

Wacatalunya hao walikuwa ugenini hapo jana, huku wakikabiliwa na majeruhi kwa wachezaji wao muhimu akiwemo Kounde, Araujo, Frankie De Jong na wengine ambao umeifanya Barca kuwa na wasiwasi.

 

Xhavi: "Lewandowski Ndiye Mfungaji Bora Duniani".

Vijana hao wa Camp Nou wameendelea kufanya vizuri kwenye mechi zao zote na mpaka sasa kwenye mashindano yote wamepoteza mechi moja tuu ambayo ni ya Klabu Bingwa na wapo nafasi ya kwanza kwenye msimamo, huku wakiwa mbele mchezo mmoja dhidi ya wapinzani wao Real Madrid.

Acha ujumbe