Yaliyojiri Ligi ya Mabingwa

Baadhi ya klabu zimeshafanikiwa kukata tiketi ya kusonga mbele kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya michezo iliyopigwa hapo jana ya kuwania tiketi ya hatua ya 16 bora ya kusonga mbele katika michuano hiyo. Nafasi hiyo imesukuma klabu nyingi kubwa kuweza kupata nafasi hiyo.

Ndani ya mechi zilizopigwa hapo jana kuna rekodi nyingi zimetengenezwa ambazo zinaendelea kuifanya michuano hiyo kuonekana kuwa bora siku hadi siku. Hata klabu zile ambazo zilikuwa kwenye hatari ya kushuka kwenye michuano hiyo zimefanya mageuzi na kushinda mechi zake.

Katika mechi ya Barcelona ambao walicheza na Inter Milan nyota wa klabu hiyo Ansu Fati amekuwa nyota chipukizi kufunga bao ndani ya michuano hiyo na kuifanya Barcelona kuwaondoa kwenye michuano hiyo Inter ambao wapo chini ya Conte na kufanya safari yao ndani ya michuano hiyo kukomea hapo wakiwa wamemaliza kwenye nafasi ya tatu na kuwaacha Dortmund kusonga mbele.

Liverpool ambao walikuwa katika hatari ya kuondoshwa kwenye michuano hiyo wamepindua meza mbele ya Salzburg na kuweza kuondoka na ushindi wa magoli mawili ambayo yalishushwa pale Salah alipoweza kufunga goli la ajabu sana na kuwafanya kuungana na Napoli ambao nao wamekata tiketi ya kusonga mbele.

Lyon ambao walionekana kabisa kuondoshwa kwenye michuano hiyo waliwa nyumbani mbele ya Leipzig, walifanikiwa kulazimisha sare ya 2 – 2 baada ya ushindi wao kuwa mgumu sana. Kikosi hicho kilipata nafasi ya kusonga mbele baada ya goli la Depay alilofunga katika dakika za lala salama za mechi hiyo na kuwawezesha kusonga mbele zaidi.

Chelsea apenya

Chelsea ameweza kusonga mbele katika michuano hiyo mbali na kuchukuliwa kwamba isingekuwa rahisi kwake kusonga mbele kwenye michuano hiyo lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa na ilivyodhaniwa. Wamesonga mbele wakiwa alama sswa na Valencia ambaye ndiye ameshika usukani wa Kundi lao kwa kumtupa Ajax nje kwa tofauti ya alama moja pekee.

Yajayo

Matokeo mengine yanasubiriwa katika mechi zitakazopigwa leo ili kujua nani ataweza kupambana na nani kusonga mbele kwenye hatua ya nane bora. Baada ya michezo ya leo, droo itachezeshwa mapema sana na kupangwa kwa klabu ambazo zitachuana kusuka pacha ya kucheza nazo.

Makala iliyopita
Makala ijayo

2 Komentara

    Nomaaa sanaaaaa

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe