Michuano ya Euro bado inaendelea na kwa sasa kila taifa linatafuta nafasi ya kujikongoja ili kupata angalau upenyo wa kusonga mbele zaidi huku baadhi ya nchi zikiwa tayari zimekata tiketi ya kusonga mbele kwenye hatua hizo za makundi kwa kukusanya alama nyingi ambazo haziwezi kufikiwa na wengine.
Timu ya taifa iliyokuwa ikiepewa nafasi kubwa ya kufanya makubwa zaidi kwenye michuano hiyo imepoteza mchezo wake mbele ya Jamhuri ya Czech ambao mbali na kwamba hawana majina makubwa mengi ndani ya kikosi chao waliweza kumudu kuchukua alama kwa Waingereza hao. Katika hatua hiyo kikosi cha Southgate bado kina jambo la ziada kufanya ili kuweza kujiwekea nafasi nzuri ya kuweza kufika pale wanapotaka.
Ukraine ambao wapo kundi moja na Ureno na ambao wanawapa maumivu ya kichwa Ureno waliibuka na ushindi ndani ya mechi yao pale walipowararua kwa magoli mawili Lithuania ambao kwa hakika hawajawa na mwendelezo mzuri sana kwenye mashindano hayo.
Ureno ambao wamekuwa wakitoa dozi mara nyingi na wakiwa katika hatua ya utetezi wa nafasi yao ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo wameibuka na ushindi wa magoli 3 – 0 mbele ya Luxembourg ambao hawakuwa katika ubora wowote kuweza kuleta ushindani kwenye mechi hiyo.
Mbali na ushindi huo kocha wa Ureno, Santos anaonekana kutokuridhishwa kabisa na kiwango cha vijana wake kwa kusema kwamba hawakuwa katika hali ya kimchezo kabisa japo wamepata ushindi na kikosi chake kimecheza mchezo wa ajabu sana ambao kwake hajaufurahia na kuona wana kubwa zaidi la kufanya ili kurudi kwenye ushindani. Nyota wa taifa hilo, Ronaldo ameendelea kuwa mwiba usioisha makali mara baada ya kuwapa ushindi Ureno na kuwa sehemu ya mafanikio ya taifa hilo ambalo linaonekana kuwa na kizazi cha pekee kwa siku za usoni katika soka.
Safari ya michuano hiyo bado ni ndefu sana na kila mmoja ana nafasi ya kufanya vizuri kwa wakati huu ili kujiweka sawa kusonga mbele. Swali bado ni zito juu ya nani ataweza kuibuka katika makundi na kufika hatua ya kutawazwa kuwa bingwa wa michuano hiyo Ulaya?
Povel
Habar njema