Yanga Inasubiri Mshindi Kati ya Simba na Azam Kwenye Nusu Fainali FA

Yanga jana walifanikiwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa Kombe la FA baada ya kutoka nyuma na kuwachapa Kagera Sugar mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

Hii ina maana kuwa sasa Yanga wamefufua matumaini ya Issa Liponda,Dar es Salaamkushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao ambapo sasa watatakiwa kucheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya mshindi wa leo kati ya Simba na Azam.

Kagera Sugar ambao wapo nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara walifanikiwa kuwa wa kwanza kujipatia bao kupitia kwa kiungo wao matata Awesu Awesu katika dakika ya 19 ya mchezo, ambaye alifunga kiufundi baada ya kumhadaa kipa wa Yanga, Metacha Mnata, kuwa anapiga krosi na mpira ukajaa wavuni.

Kipindi cha kwanza chote Kagera walionekana kuwa bora huku wakitawala zaidi kwenye eneo la kiungo na Yanga wakipoteza mipira mingi.Mbali na bao hilo, beki wa timu hiyo David Luhende alipiga shuti kali katika dakika ya 45 baada ya kupiga shuti kali lilopaa juu ya lango la Yanga.

Nafasi pekee ambayo Yanga wanaweza kuijutia kipindi cha kwanza ni ile waliyopata dakika ya 43, ambapo kiungo wao Feisal Salum alipiga kichwa kikapaa juu.Kipindi cha pili, Yanga walionekana kuwa bora baada ya kuingia Mrisho Ngassa, ambapo katika dakika ya 51 tu alitoa pasi safi kwa mshambuliaji wa Yanga, David Molinga ambaye aliisawazishia timu yake bao safi.

Baada ya bao hilo, Yanga walionekana kuwa bora na kutawala mchezo lakini katika dakika ya 77 walipata penalti ambayo ilionekana kama vile Ngassa ameangushwa nje ya 18 na Juma Said Nyosso, lakini mwamuzi akaamuru ni penalti iliyofungwa na Deus Kaseke ambaye aliweka mpira huo kimiani na kuipatia Yanga bao la pili Hata hivyo, dakika chache baada ya bao hilo, Awesu Awesu alipewa kadi nyekundu ikionekana kama alijibizana vibaya na mwamuzi wa mchezo huo.

Katika mchezo mwingine, Wabishi wa Kusini, timu ya Namungo ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwenye mchezo wa mapema baada ya kuichapa Alliance mabao 2-0.

Mabao ya Namungo yalipachikwa kimiani na Bigirimana Blaise kwa penalti na George Makang’a aliyefunga bao la kideo ndani ya 18, watavaana na Sahare au Ndanda kwenye hatua ya nusu fainali.

34 Komentara

    Kwa Jana ilikuwa furaha sana kwa mashabiki wa yanga ingawa walisua suwa mechi zilizo pita hata hivyo katika mchezo wa Jana namungo alionekana amepata penalty Ila ile sio penalty ukiangalia kwa makini. Pongezi sana yanga

    Jibu

    Yanga inapewa nafasi kubwa ya kushinda na kusonga mbele hatua inayofuata kutokana na kiwango bora ilichokuwa nacho hivi sasa lakini pia kuwa juu kwa kiwango cha soka ambayo kwa sasa inapambana kutoka katika soka la ridhaa kuja la biashara.
    Kitu kingine kinachoifanya Yanga kupewa nafasi ya kushinda na ubora wa kikosi ilichonacho ambacho kinaundwa na nyota kutoka mataifa saba tofauti ambayo ni Togo, Niger,DR Congo, Rwanda,Zimbabwe Burundi na Tanzania
    Mbali na kuwa na nyota kutoka mataifa hayo saba lakini hata gharama ya usajili iliyotumika
    Pamoja na hayo Yanga imekuwa ikijizolea sifa kubwa kwa kila mwaka kushiriki michuano ya kimataifa kama siyo hiyo ya Ligi ya mabingwa basi itakuwa ile ya Kombe la Shirikisho
    Kabla ya fainali za mwaka huu mara ya mwisho timu hiyo kushiriki ligi ya mabingwa Afrika ilikuwa ni mwaka juzi ambapo timu hiyo ilitolewa na National Al Ahly kwa changamoto ya mikwaju ya penalt baada ya kutoka sare ya kufunga mabao 1-1 Yanga wakishinda bao 1-0 nyumbani na katika mchezo wa marudiano Ahl nao wakashinda 1-0 na kuamuriwa zipigwe penati.
    Kabla ya hapo Yanga iliitoa Komorizone ya Comoro, kwa idadi kubwa ya mabao kiasi cha kumfanya winga mrisho Ngasa kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga Hart trick mbili katika michezo yote miwli ya nyumbani na ugenini.
    Baada ya hapo msimu uliofuata Yanga ilikosa ubingwa ikamaliza msimu nafasi ya pili ambapo ilishiriki michuano ya kombe la Shirikisho mwaka jana na safari hii ilionekana kujipanga kiasi kwa kufika hadi raundi ya tatu kabla ya kutolewa na Etoile du Sahel kwa mabao 2-1.
    Mwaka 2012 Yanga ilikuwa bingwa wa Tanzania na kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa safari hiyo iliaga mapema michuano hiyo kwani mchezo wa raundi ya kwanza ilipangiwa Zamalek ya Misri na haikuweza kufa dafu baada ya kutupwa nje kwa jumla ya mabao 2-1
    Kwa historia hii Kati ya azam na Simba wanatakiwa kujipanga tena sana kutafuta ubingwa maana ukicheza na timu ya kimataifa ya wananch unatakiwa ujipange maana KMC wanatujua hata kagera jana waliona mziki wa yanga hivyo bas tunapenda kutangaza mapema ubingwa n wetu
    # YANGA oyeeeee

    Jibu

    Haya mambo ya yanga ni kuumizana vchwa tu

    Jibu

    Asante meridianbet kwa taarifa

    Jibu

    Kuna watu wasipoiongelea Yangu kwa siku hawajisikii vizuri kwa kiwango alichoonesha jana lazima wewe ukubari matokeo ,mkubwa mkubwa bwana usimchezee

    Jibu

    Game ya Jana ilikuwah habar njema kwa mashabik wa yanga kwa kutinga hatua ya nusu fainali kwa upande wa mkurukumbi kagera sukari lawama zote kwa mwamuzi kwa kushndwa kusimamia sheria kumi na 17 za mpra wa miguu na kufanya maamuz yaliyopelekea kukandamizah upande mmoja wa kagera sukari ila ngoj tuone mtanange wa leo wa matajir wa jiji la dar es salaam azam fc na Simba wazee wa msimbazi ,huku SIMBA wakitaman kushndah leo iliwawez kulipizah kikas kwa kufungwa kwny kombe la ligi(vpl) ngoj tuone mtanange utakuwaje hii leo AZAM fc Matajir wa jiji la Dar vs SIMBA wa zee wa Msimbazi Kick off 7:00pm Kwa MKAPA STADIUM (kwa mchina )

    Jibu

    Sisi Simba tunawataka Sana hao yeboyebo#meridianbettz

    Jibu

    Yanga. Itafanikwa tu kuchukua ubingwa aababu ni kombe ambalo inalipigania kwa hali na mali

    Jibu

    Viva yangaa ahahaaaaaaaaa…ongera kwao

    Jibu

    Wanaomba Simba ifungwe tusikutane nao,Wazee wa kubebwa#Meridianbettz

    Jibu

    Licha ya refaree kualib mchez lkn match ilikua nzur team zote zilionyesh uwez

    Jibu

    Wana yanga tunapenda Sana ndugu zetu wanao jiita wao simba washinde mechi Kati yao na wana lamba lamba Ili tumrudishe mke wetu tulio muoa kwa Mara ya kwanza na kumuacha sasa tumemkumbuka tena kwa mambo aliyo tufanyia kwa sababu hatujawahi kuoa mke mvumilivu na mwenye madeko Kama yeye azamu tunaomba mturudishie mke wetu tunataka kurenew ndoa kwa Mara ya pili

    Jibu

    Hahaha hapo matokeo tunayo mashabiki yanga waache waendelee kusubiria matokeo

    Jibu

    Maoni:Asante kwa taarifa

    Jibu

    Shukrani kwa ujumbe

    Jibu

    Hata mkiandika MAKALA ndefuu Sana lakini Kama mtaktana na Simba mnyama mtapigwa 5-0 maana yanga hamna noya zaidi ya kubebwa

    Jibu

    Wazee wakubebwa hawatumiizi kichwa

    Jibu

    Yanga wafanye kazi ya ziada kwa kuwashinda Simba ila hawatoweza kuwavaa mabingwa wa nchi

    Jibu

    Ahsant meridian kwa habari

    Jibu

    Duuh kwanza nicheke eti yanga hapa mpira tuu simba oyeeee simba hatubebwi

    Jibu

    Simba hatuna mpinzan

    Jibu

    Hapo tutasubilia dakika 90 tu ndo jibu litapatikana

    Jibu

    simba babalao

    Jibu

    Simba lazima wamchape yanga

    Jibu

    Yanga mbeleee

    Jibu

    Nusu fainali ya FA naona simba na yanga

    Jibu

    Hatari sana.

    Jibu

    FA lazima iende kwa simba tu

    Jibu

    Asanteni kwa taarifa

    Jibu

    Mh!

    Jibu

    Final ni SIMBA vs NAMUNGO … bingwa anachukua Simba namungo mshindi wa pili ….ndio maaana league ya Bongo siipendi

    Jibu

    Yanga daima mbele nyuma mwiko

    Jibu

    yanga oyeer

    Jibu

    Akuna lolote wa subilie mchezo utao chezwa siku hiyo wajipange kisawa sawa pata chimbika sikuhiyo mtoto atumwi dukani dadeki Simba Wana lihua jitu sikuhiyo

    Jibu

Acha ujumbe