YANGA KUFUNGUA PAZIA LA KIMATAIFA CHAMAZI

Kwa taarifa za awali ni kwamba mechi za kimataifa za hatua ya awali kati ya Vital’O ya Burundi na Yanga SC ya Tanzania, zinaweza kuchezwa hapahapa Tanzania kutokana na changamoto zisizo za kimichezo,

Hivyo Vital’O wanatazamia kucheza michezo yao ya awali kwenye viwanja walivyoviomba nje ya Burundi ambapo uwanja wa KMC na Azam Complex ni miongoni mwa viwanja hivyo.

Kama itakuwa imekaa vizuri basi Yanga watapata unafuu wa kucheza mechi zote wakiwa na umati wa Mashabiki wao.

Acha ujumbe