Yanga Kupata Mbadala wa Songne Dirisha Dogo.

Klabu ya Yanga SC imeweka wazi kuwa kwa sasa ipo kwenye hesabu za kumsaka mbadala wa mshambuliaji wao Yacouba Songne ambaye anatarajiwa kuwa nje kwa msimu mzima wa 2021/22.

 

Songne aliumia mguu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga SC dhidi ya Ruvu Shooting, Novemba 2,2021 kwa sasa bado anapewa matibabu ili aweze kurejea kwenye hali yake ya kawaida.

Akizungumza siku ya Jumatatu Mtendaji Mkuu wa Yanga SC, Senzo Mbatha alisema kuwa wanatarajia kufanya usajili mdogo kwenye dirisha dogo ili kuweza kuwa imara zaidi.

“Ikifika dirisha dogo nina amini kwamba tutafanya usajili lakini sio mkubwa sana,tuna mchezaji kama Yacouba, (Songne) huyu bado aliumia hivyo tutafanya utaratibu kumpata mchezaji mwingine ambaye atakuja.

“Unajua kikosi imara kinahitaji wachezaji wazuri na kwa namna tulivyo kila mchezaji yupo bora jambo hilo linaonekana kwani hatuna hofu tunapoingia uwanjani kucheza na timu pinzani kwa namna yoyote ile kwa kuwa kila mchezaji ana uwezo mkubwa,” alisema Mbatha.


ANZA MSIMU WA SIKUKUU NA BURST THE BANK

Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe