YANGA MZIKI UMETIMIA KUIKABILI PAMBA

VINARA wa Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, Yanga Februari 28 2025 watakuwa kibaruani kusaka pointi tatu dhidi ya Pamba Jiji.

 

Yanga baada ya mechi 21 ambazo ni dakika 1,890 wamekomba pointi 55 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 55 ikiwa ni namba moja kwa timu zenye mabao mengi ndani ya ligi.

 

Miongoni mwa wachezaji waliopo Mwanza kuelekea mchezo huo ni kiungo Mudathir Yahya, mshambuliaji Prince Dube na Clement Mzize ambao hawa wawili kila mmoja katupia mabao 10.YANGA

Miloud Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hakuna mchezo mwepesi ndani ya Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC.

 

Pamba kwenye msimamo ipo nafasi ya 11 ikiwa imekusanya pointi 22 baada ya kucheza mechi 21 huku Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 55 baada ya kucheza mechi 21.

 

Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo hautakuwa mwepesi kutokana na wapinzani wao Pamba Jiji kuhitaji pointi tatu ili kuwa kwenye nafasi nzuri ndani ya msimamo.

 

“Tunatambua kwamba wapinzani wetu Pamba Jiji wanahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu malengo ikiwa ni kuona kwamba wanakuwa kwenye nafasi nzuri hilo lipo wazi kwani hakuna mchezo rahisi hivyo tutaingia kwa tahadhari ili kupata matokeo mazuri.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.